MwanzoContactsEmail
Home Habari Habari za Kitaifa Mashangingi ya mawaziri yazua utata
BOOKMARK THIS PAGE
Mashangingi ya mawaziri yazua utata  Send to a friend
Sunday, 28 November 2010 21:05

Sadick Mtulya

WAKATI mawaziri na manaibu wawaziri wakikabidhiwa magari mapya, baada ya kuapishwa Jumamosi iliyopita, serikali imeibuka na kusema sio mapya ni ya zamani.
Kauli hiyo inaibua utata kutokana na kuwa baada ya kuapishwa viwanja vya Ikulu na Rais Jakaya Kikwete, kila waziri alikabidhiwa dereva mpya na gari jipya aina ya Toyota GX V8, badala ya gari aina ya Toyota VX V8 iliyokuwa ikitumiwa na mawaziri waliopita.

Ununuzi wa Toyota GX V8 mpya, unashiria serikali bado haijawa tayari kuunga mkono msimamo wa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ambaye amekuwa akisikika akitaka kusitishwa ununuzi wa magari ya kifahari ili kupunguza matumizi ndani ya serikali.

Toyota GX V8 moja huuzwa kati ya Sh210 milioni hadi Sh240 milioni, hukuToyota VX V8 moja inauzwa sio chini ya Sh180 milioni.
Akizungumza na Mwananchi jana, Katibu Mkuu wa iliyokuwa Wizara ya Miundombinu, Omari Chambo, alisema magari hayo sio mapya na kwamba, yaliyotumiwa na mawaziri waliopita.
Rais Jakaya Kikwete ameigawanya iliyokuwa Wizara ya Miundombinu na kuwa wizara mbili; Wizara ya Ujenzi na Wizara ya Uchukuzi.

“Yale magari sio mapya, yalikuwepo. Kwanza uliyaona au unasema tu, hamjayachunguza vizuri jamani, fanyeni uchunguzi,’’ alisema Chambo na kukata simu.
Mawaziri wote na baadhi ya manaibu walikabidhiwa magari hayo (GX V8), huku manaibu wengine wakikabidhiwa VX V8.
Sababu ya baadhi ya manaibu mawaziri kukabidhiwa VX V8 badala ya GX V8, ni kutokana na kutokamilishwa kwa taratibu za kutokamilika.

Mmoja wa manaibu mawaziri (jina tunalo), alikabidhiwa VX V8 iliyokuwa ikitumiwa na aliyekuwa Waziri wa Maendeleo ya Mifungo na Uvuvi, John Magufuli, ambaye sasa ni Waziri wa Ujenzi.
Gazeti moja la kila siku (si Mwananchi) limeeleza kuwa ununuzi wa magari hayo, umegharimu serikali Sh9.3 bilioni na kwamba, takwimu za iliyokuwa Wizara ya Miundombinu zinaonyesha kuwa hadi kufikia mwishoni mwa mwaka wa fedha wa 2005/06 magari makubwa ya kifahari yapatayo 6,000 yalikuwa yamenunuliwa na serikali kwa gharama inayokadiriwa kufikia Sh160 bilioni.

Miongoni mwa magari hayo ni Toyota Land Cruiser (VX/ GX V8, Prado) yapatayo 1,655, Nissan Patrol na Land Cruiser 885, Mitsubishi Pajero 400 na mengineyo.
Tangu kipindi cha serikali ya awamu ya tatu chini ya Rais  mstaafu, Benjamin Mkapa, kumekuwepo na mjadala kuhusu matumizi makubwa ya serikali hasa katika ununuzi wa magari ya kifahari kutokana na kuendeshwa kwa gharama kubwa.
Wadau wengi wanataka viongozi watumie magari ya kawaida kama ilivyo kwa nchi ya Kenya na Rwanda


Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
Reddit! Del.icio.us! Mixx! Free and Open Source Software News Google! Live! Facebook! StumbleUpon! TwitThis Joomla Free PHP
 

Comments 

 
0 #14 2010-11-30 02:34
nchi ni masikini lakini viongozi wetu inaonekana hawali tambui hili ,hawajui hali kama hii ni changamoto ya kuchochea yavitendo vya uhalifu mbalimbali kama vile ujambazi nk.Kwani inakatisha tamaa,walim wallio watoa mbali hawana hata baiskeli au naulli za kupanda daladala kuwapeleka mahospitalini.du!full joka la mdimu
Quote
 
 
0 #13 2010-11-30 02:21
hii ni tabia ya mtanzania kwani utasikia jamaa ana hela wakati ana zero investimate...... watanganyika hatuna tabia ya kuwekeza kwa ajili ya watoto na wajukuu wetu tumebakia katika ponda mali kufa kwaja..... tutayasikia maendeleo kwenye radio na luninga hadi hapo tutakapo sema STOP na kuanza kuwekeza kwa ajili ya feature...... remember ..... ASK NOT WHAT THE GOVERNMENT CAN DO FOR YOU ASK WHAT YOU CAN DO FOR THE YOUR PEOPLE....
Quote
 
 
0 #12 2010-11-29 19:54
JK ALIINGI IKULU KUKIWA NA MA-BENZI. HALAFU YAKALETWA MA-BMW NA KABLA YA [NENO BAYA]LIZA MIAKA YAKE MITANO, YAKALETWA MA-TOYOTA!
Quote
 
 
0 #11 2010-11-29 19:36
Ni aibu kwa nchi yetu tukufu.
Kwa nini tununue magari kila baada ya miaka mitano? Kuwe na mkakati madhubuti wa kuyatunza magari hayo ili hata viongozi wajao waweze kuyatumia.

Walimu na wahudumu wa afya bado wanalipwa mishahara ya chini mno hata ukifananisha tu na nchi za Afrika Mashariki.

Tumlilie nani watanzania?
Quote
 
 
0 #10 2010-11-29 16:05
Quote
 
 
+2 #9 2010-11-29 15:04
Ivi kwanini hizo pesa zisipelekwe kwenye wizara ya afya, ambako watu wanapoteza maisha kwa kukosa huduma,nahakuna vitendea kazi vya kutosha Jamani embu muwe na huruma na hizo pesa zetu, Nakuwa sielewi kabisaa mnaposema Tanzania ni nchi maskini wakati Mawaziri 50 kumiliki magari yenye thamani ya Tshs 9.3 bilion je huu ni ungwana????????????????????????
Quote
 
 
+2 #8 2010-11-29 14:10
Jamani kwa nini wasiboreshe usafiri wa umma ili waepuke kununnua hayo magari ya kila baada ya miaka mitano.Magari ya serikali yapo mengi ingekuwa ni vizuri kama wangetufikiria sisi wanacni tunaoishi madongo kuinama ile foleni ndani ya vipanya hakuna hewa hakuna. Hizo pesa angalau wangefikiria kujenga barabara za kisasa ili punguza foleni au kupatia wananchi maji safi ili tuondokane na kipindupindu. Ni aibu nchi masikini lakini viongozi wake wanatembelea magari ya kifahari kuliko viongozi wa nchi tajiri na ndio wao wanatuma pesa za misaada ili kusaidia bajeti ya nchi. Hivi ni lini viongozi wetu wataanza kuwajali wananchi wao?????
Quote
 
 
+2 #7 2010-11-29 13:32
Kwa serikali hii ya Jk and mabest zake. Hatutegemi zaidi ya kutanua na kuindana.
Quote
 
 
+2 #6 2010-11-29 12:05
Huo ndio uhayawani wa sisiem
Quote
 
 
+3 #5 2010-11-29 10:43
Watanzania kila mmoja wetu anayaona matatizo ya Serekali kwa ujumla wake. Kelele zetu kuhusu kupunguza matumizi wanadai haziwanyimi usingizi. Kazi kwetu 2015.Kura zetu kama kwaida apewe mwenye uelekeo wa kutukomboa.
Quote
 
 
+3 #4 2010-11-29 10:26
Kwa kweli matanuzi yanatisha huku hospitali hata zile za mkoa zikikosa madawa hata ya kawaida kama vile Potassium pamanganet ni aibu kwa viongozi kuishi kianasa huku mambo muhimu kama maabara nyumba za walimu zikiachwa kujengwa kwa kisingizio cha ukosefu wa fedha.lakini wananchi ndio hasa wanatakiwa kuhoji haya wakati wa kampeni.Inasikitisha kuona kwamba badala ya wananchi kuuliza maswali wanabaki kucheza ngoma tu na kushangilia hili ni tatizo kubwa sana kwa maendeleo ya taifa .
Quote
 
 
+3 #3 2010-11-29 08:49
Kama bado CCM ipo Madarakani Mtanzania yeyote asitegemee serikali kuweka mkazo wa kupunguza matumizi kwani ndio stail ya utawala wao na lengo ni kutesa kwa zamu.Mambo mengine ni ya kiasiasa tuu hakuna implementation.
Quote
 
 
+2 #2 2010-11-29 08:42
MMh! Kwa hali hii kweli Nchi yetu kutakuwa na Maendeleo!! Hapa hebu tizama kidogo katika hili jiji la Dar-es salam,Mama zetu wanahangaika na Ndoo za maji kuyafata masafa marefu na huko Vijijini halikadhalika lkn Serikali hii kama Hizo Milio 240 walizotumia kununulia Gari moja Ya GX V8 ....Jee Pesa hizo vingechibwa Visima vingapi??? Mhh! kweli Tanzania tutafika tunapokwenda!!!
Quote
 
 
+2 #1 2010-11-29 08:41
nchi masikini lakini viongozi wetu wanapenda starehe utafikiri bndo magari yaepushayo ajali kumbe hakuna lolote gari moja zaidi ya milioni 200 huu ni wizi wa hela za kodi ya wananchi,baraba ra kibao hazipitiki lakini wanishia kukalia magari hayo,inasikitis ha sana wapenda starehe nchi ya Rwanda sasa inakuja juu na ni miaka ya juzi tuliwashuhudia wakiwa katika hali mbaya ya vita ila viongozi wetu ni wa[NENO BAYA] sana.
bila mikimiki hatatufika lazima tuhoji huu ni ufisadi kabisa
Quote
 

Add comment

Tumia jukwaa ili kutoa maoni ambayo yatasaidia kulijenga taifa letu. Kumbuka, maoni yako yatapitiwa kwanza kabla hayajarushwa hewani!!!!!!


Banner
Banner
Banner