MwanzoContactsEmail
Home Habari Habari za Siasa Chadema wamkamata Mkuu wa Wilaya Igunga
BOOKMARK THIS PAGE
Chadema wamkamata Mkuu wa Wilaya Igunga  Send to a friend
Thursday, 15 September 2011 21:40

Boniface Meena na Daniel Mjema, Igunga
VURUGU zimezuka jana katika Kata ya Isakamaliwa, wilayani Igunga zikiwahusisha viongozi wa Chadema na Mkuu wa Wilaya ya Igunga, Fatma Kimario.Katika sakata hilo, wanachama wa Chadema walimkamata Mkuu huyo wa Wilaya kwa tuhuma za kuendesha mkutano wa ndani na watendaji wa serikali za vijiji, wakati akijua kuwa kulikuwa na mkutano wa kampeni za chama hicho karibu na eneo hilo.

Msafara wa Chadema ulifika katika eneo la kampeni saa 8.00 mchana na kabla mkutano haujaanza, Meneja Kampeni wa chama hicho, Sylivester Kasulumbai, aliwaambia waandishi wa habari kuwa mkuu wa wilaya ya igunga alikuwa akifanya kikao cha ndani katika eneo hilo kinyume na taratibu, hivyo wanakwenda kumshughulikia.

Kasulumbai ambaye ni Mbunge wa Maswa Mashariki akiwa na Mbunge wa Viti Maalum, Susan Kiwanga, baadhi ya wananchi na vijana wao, walifika katika ofisi ya Mtendaji wa Kata kulikokuwa kunafanyika mkutano huo na kuanza kuhoji aliko Mkuu huyo wa Wilaya.

Mmoja wa wananchi alimnyooshea kidole mama ambaye alikuwa amekaa mbele na kusema; “..yule ndiye Mkuu wa Wilaya”.Kundi hilo la vijana na viongozi wa Chadema, waliingia katika ukumbi huo na kumtoa nje mama huyo huku wakimtaka aeleze kwa nini anafanya vikao vya ndani katika Kata hiyo wakati anajua kuwa chama hicho kilikuwa na mkutano katika eneo hilo.

Kitendo hicho kilizua purukushani na kutokuelewana kati ya waliokuwa kwenye mkutano wa ndani na viongozi wa Chadema, jambo lililovuta umati mkubwa wa watu.

Maelezo ya DC
Baadhi ya vijana wa Chadema walikuwa wamewashikilia watu waliokuwa wakishiriki mkutano huo huku mama huyo akitolewa nje na kuketishwa kwenye kiti alitakiwa atoe maelezo kuhusu mkutano wake.

Baada ya kukaa kwenye kiti huku akionekana kuchanganyikiwa, alisema yeye ni Mkuu wa Wilaya ya Igunga, jina lake ni Fatma Kimario na kwamba, hakuwa na taarifa za mkutano wa kampeni za Chadema.

“Sina ratiba, iko katika ofisi za halmashauri, hivyo sikujua kama kuna mkutano hapa, hata hivyo watu walikuwepo niliwaruhusu waende mkutanoni na mimi nilikuwa naondoka sasa hivi,” alisema na kuongeza:

“Nilichokuwa nafanya ni mkutano wa viongozi wa serikali kwa ajili ya kuangalia hali ya mifugo inayoibwa sana, elimu kwa wote hasa watoto na ujenzi wa nyumba bora na masuala ya amani”.

Kimario aliwasihi wafuasi wa Chadema kusoma karatasi ya ajenda ili wafahamu kilichokuwa kikijadiliwa kwenye kikao hicho.

Karatasi aliyokuwa akiizungumzia Mkuu huyo wa Wilaya ilikuwa na ajenda tano za kikao hicho ambazo ni; Uhamishaji wa mifugo; Kuwa na choo chenye ubora na nyumba bora; Elimu;  Mipaka ya shule na ajenda ya mwisho ilikuwa Uchaguzi mdogo wa ubunge Jimbo la Igunga.

Hata hivyo mbunge Kiwanga alimtaka mkuu huyo wa wilaya aeleze tangu lini kikao cha viongozi wa serikali kikahudhuriwa na wazee maarufu na mabalozi wa nyumba kumi, swali ambalo lilionekana kumchanganya mkuu huyo wa wilaya kwa kutoa majibu tata.

Mkutano wa Chadema
Wakati hayo yakiendelea, mkutano wa kampeni ulikuwa nao ukiendelea, hivyo viongozi hao wa Chadema walimtaka DC huyo afike kwenye mkutano huo ili aweze kuonana na Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa.

Kimario alikubali, lakini akataka dereva wake atangulize gari na kwamba yeye angefuata. “Nitakwenda kwani napaswa kuwepo pale kama msimamizi wa usalama, sijahudhuria mkutano wowote hivyo nitakwenda,” alisema.

Akizungumzia tukio hilo kwenye mkutano wa kampeni, Dk Slaa alisema wakuu wa wilaya na mikoa kufanya mikutano wakati wa kampeni ni kinyume cha sheria, hivyo Kimario alienda kuanzisha vurugu.

“Hapaswi kufanya mkutano wowote hapa hasa akijua kuwa sisi tuna mkutano wa kampeni na yeye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama wa Wilaya,” alisema Dk Slaa na kuongeza:

“DC anafanya nini huku wakati hiki ni kipindi cha uchaguzi au ndiyo wanapanga mikakati ya uchakachuaji halafu wanadai sisi ndiyo tunaofanya vurugu?”

Mkutano wa kwanza na wa pili wa Chadema, hakukuwa na ulinzi wa polisi kama ilivyokuwa kwenye mikutano mingine.

Askari wamwagwa
Wakati gari la waandishi wa habari likirejea mjini Igunga, lilipisha na magari mawili ya polisi yakiwa yamejaa askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), ambayo yalikuwa katika mwendo kasi yakielekea eneo la tukio.

Magari hayo yalifuatiwa kwa nyuma na gari aina ya Toyota Landcruiser ambalo lilikuwa na vioo vyeusi yote yakiwa yamewasha taa kuashiria hali ya hatari.

Hata hivyo polisi wilayani Igunga kupitia kwa Mkuu wake (OCD), Issa Maguha, waliliambia Mwananchi kuwa hawakuwa na taarifa ya tukio hilo na kwamba magari hayo yalikuwa katika doria za kawaida.


CCM yawaangukia wananchi

Katika hatua nyingine CCM kimewaangukia wananchi wa Igunga kikiwataka kuacha jazba na hasira kwani madhara ya kuchagua mbunge kwa chuki yataligharimu jimbo hilo kwa miaka minne ijayo.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Katibu wa NEC ya CCM Uchumi na Fedha, Mwigulu Nchemba wakati akihutubia mkutano wa kampeni katika kijiji cha Usongo kata ya Nyandekwa kinachoaminika kuwa ngome ya Chadema.

Habari zilizopatikana kijijini hapo kabla ya kuanza kwa mkutano huo zilidokeza kuwa Chadema walitangulia kufanya mkutano wa kampeni kijijini hapo na kumwaga ‘sumu’ ili wananchi waichukie na wasiichague CCM.

Akihutubia mkutano huo, Nchemba alirudia mara kadhaa kusema, “shusheni jazba” na “punguzeni hasira” ambayo ilitafsiriwa na wengi kuwa ni kujaribu kung’oa mizizi ya Chadema.

Katibu huyo alisema Chadema kimekuwa kikipandikiza chuki kwa wananchi kwamba Serikali ya CCM haijafanya lolote katika kipindi cha miaka 50 ya Uhuru. Alisisitiza kuwa huo ni uongo wa karne unaopaswa kupuuzwa.

“Kuwa na vuguvugu la kifikra inaruhusiwa na pia kuwa na mtizamo tofauti inaruhusiwa lakini si katika kipindi hiki ambacho wananchi wa Igunga wanahitaji mgombea wa CCM kuliko kipindi kingine chochote,” alisema.

Nchemba aliendelea kusema: ”kwenye uchaguzi mdogo nawaombeni mshushe jazba.…hata kama ulikuwa tayari na mlengo fulani, basi badilika kwa manufaa ya wana Igunga…, tusishabikie vyama bali tujadili hoja”.

Katibu huyo ambaye pia ni Mbunge wa Iramba Mashariki, aliwasihi wananchi wa kijiji hicho na Jimbo la Igunga kuacha kushabikia mambo ya maendeleo kama wanavyoshabikia timu za soka hata ambazo hawazijui.

Kwa upande wake, mgombea Ubunge wa CCM, Dk Dalaly Kafumu aliahidi kusimamia mradi wa kuvuta maji kutoka Ziwa Victoria hadi Igunga kupitia majimbo ya Kahama na Nzega.

Dk Kafumu aliahidi kutumia utaalamu wake wa madini kuhakikisha kuwa wachimbaji wadogo wanatengewa maeneo yenye madini katika jimbo hilo na kutatua tatizo na kero ya muda mrefu ya daraja la Mbutu.

Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
Reddit! Del.icio.us! Mixx! Free and Open Source Software News Google! Live! Facebook! StumbleUpon! TwitThis Joomla Free PHP
Last Updated on Saturday, 17 September 2011 08:04
 

Comments 

 
0 #150 2011-09-19 12:56
wewe sema piga hao na endelea kuwashangilia ipo siku watakuja kumpiga mama yako utaona uchungu wake unakuwa kama si binadamu
Quote
 
 
0 #149 2011-09-19 12:44
chadema hamshindi hata kwa mapanga palipo tokea janga la kuzama kwa meli kule zanzibar kama nyie kweli ni wapenda wananchi mbona hamukusitisha kampeni, tumesha wastukia hamna upendo wa dhati na inchi hii hamna jipya ccm tunasema amani na upendo ni jambo la kwanza lakini kwenu amani na utulivu havina maana vinaweza kusubili WATANZANIA TUWAANGALIE CHADEMA NA TANZANIA WANAYOHITAKA YAANI VURUGU TUUU
Quote
 
 
0 #148 2011-09-19 09:37
Ni udhalilishaji mkubwa kwa cc wanawake tunaojistahi na kujiheshimu. kijana huyo aliyemshika mkono mm wa wenzie km ni wake angejiskiaje? hapakuwa na njia mbadala ya kumheshimu tena kwa cheo chake mama huyo? wahusika waadhibiwe iwe funzo kwa wengine.
Quote
 
 
0 #147 2011-09-18 14:31
Wananachi wa Igunga msidanganywe na huyo Kafumu kuwa, wachimbaji wadogo wadogo watatengewa maeneo. HUO NI UONGO KABISA, angalieni kote kwenye migodi ya wawekezaji kwa muda mrefu wanalia watengewe maeneo lakini wanafukuzwa kama wakimbizi. Wakivumbua dhahabu sehemu ya pori, baada ya muda unasikia eneo hilo ni la mtu fulani ana leseni na hati ya kumiliki! KAFUMU na CCM yake ni WAONGO pigeni chini hao!
Quote
 
 
0 #146 2011-09-18 09:11
Jaman Tanzania tunakwenda wap? kama mama mzima anatharirishwa hivi na mtoto mdogo kama mwanae na watoto wake wanajisikiaje wanavyomkokota mama yao CHADEMA msilifumbie macho hili litawachafua CCM watapata pa kusemea
Quote
 
 
0 #145 2011-09-17 21:22
chadema fanyeni kazi ya kuirudisha TZ katika mstari,ufisadi na kujivua gamba ni mwanzo wa kufa kwa ccm.ALL DA BEST CHADEMA.
Quote
 
 
0 #144 2011-09-17 21:15
Hata kama dc alikosea,bado ilipaswa haki zieshimiwe. Two wrong don't make one right. Amekosea acheni sheria imhukumu. Kilichofanyika ni uzalilishaji wa kijinsia,ajabu mbunge amabaye anatetea wananchi, anaenda kumkunja mwanamke hani anamuweka uchi.
Chadema angalieni tena namna ya kuwashuulikia watu kama hao. hapo mmekosea.
Quote
 
 
0 #143 2011-09-17 10:59
hao ni mawakala wa mfumo kri na hapo bado
siku watamkamata sheikh akiwa ndani ya msikiti wao wakiwa na mkutano ktk eneo hilo
Quote
 
 
0 #142 2011-09-17 08:00
Kamanda wa polisi Maswa Magharibi alipigwa makofi na mitama na mgombea ubunge wa CCM. Je kuna mwana CCM YEYOTE ALIYELALAMIKA? AU KUNA KESI YOYOTE? Kama nyinyi wenyewe hamfuati sheria mlizozitunga wenyewe mnategemea nani azifuate? PIGA WOTE!!!!!!
Quote
 
 
0 #141 2011-09-17 07:37
Huu nu uvunjifu wa amani,hivi huyu mama alikuwa anafnya mkutano au kikao? halafu yeye kama Mkuu wa Wilaya alikuwa katika ratiba zake ninyi mnaletea mambo ya ajabu km hayo mnajichukulia sheria mkononi mkikamatwa mtasemaje,jaman i huu si ustaarabu,HUU NI UDHALILISHAJI AU MLIMUONEA KWA SABABU NI MAMA? HAPANA SERIKALI LAZIMA IFANYE KITU HAPA,HII SERIKALI MKO WAPOLE MNO NDIO MAANA WANAWATUKANA NA KUUITA SERIKALI LEGELEGE,HIVI MLIVYOFANYA KWA MAMA HUYU SIO KABISA.KAMA SIASA NDIO ZIKO HIVI BASI NCHI HII HAITAFIKA MAHALI!
Quote
 
 
+1 #140 2011-09-17 07:06
well done Chadema. Kazi ni moja tu... piga hiyo mi[NENO BAYA] kwa faida ya Tanzania. pigaaaaaa tena na tena..... Well done..... Matunda ya ufisadi wenu mnayaona sasa....
Quote
 
 
+1 #139 2011-09-17 06:58
Yah! it was ok, alistahili aongezewe na kichapo juu ili na wengine wenye njama za kushindisha ccm kibabe wajifunze. Kwa nn nyie tu kwani mna hati miliki ya nchi yetu? hata km mnayo fanyeni kazi basi, umeme hola! sukari haishikiki! chakula hakuna! alafu bado mnalazimisha kuwaongoza watu ili muwaongoze kwenye kifo au?
Quote
 
 
+1 #138 2011-09-17 06:45
baadhi ya watz ni kama vichwa vya mbu zi!! Chadema watoe taarifa kwa police unadhan polis wengemkamata huyo dc? Wameshindwa kukamata mafisad ndo maana chadema wameamua kufanya kaz iyo wenyewe. Ni dhahiri mama huyu dc kavunja sheria! Chadema hatubahatishi, tunazijua sheria za kampeni! Ccm ni wanafiki, wakandamizaji, na wakiuka sheria kene kila kitu, mpaka kuna watz walishazoea nyendo za ccm na kuzipenda! Wamekuwa ka mako ndoo ya ccm!! Chadema hatubahatishi, tunazijua sheria za kampeni! Ccm ni wanafiki, wakandamizaji, na wakiuka sheria kene kila kitu, mpaka kuna watz walishazoea nyendo za ccm na kuzipenda! Wamekuwa ka mako ndoo ya ccm!
Quote
 
 
0 #137 2011-09-17 06:43
Katika ajenda za huyu mama alizokamatwa nazo, hakutaja kitu kitwacho unemployment au ukosefu wa kazi kwa walio wengi wilayani humo.Kitendo cha kufanya mkutano huku akijua chadema nayo imo mkutanoni ni cha kihaini na kingeweza kuleta vurugu mbaya sana. Hawa ndio wakuu wa wilaya wasio jua kumgusa mwananchi kwa matendo na wala hawana habari na swala nyeti la unemployment. Hivyo huyu mama afunguliwe mashtaka haraka sana . hajui nini atendalo!
Quote
 
 
+1 #136 2011-09-17 05:00
Mkuu wa wilaya anakamatwa kama mwizi polisi wako wapi? Hawa chadema wanaweza kumwagia tindikali machoni
Quote
 

Add comment

Tumia jukwaa ili kutoa maoni ambayo yatasaidia kulijenga taifa letu. Kumbuka, maoni yako yatapitiwa kwanza kabla hayajarushwa hewani!!!!!!


Banner
Banner
Banner