MwanzoContactsEmail
Home Habari Mahakamani JK: Nikumbukwe kwa mambo nane
BOOKMARK THIS PAGE
JK: Nikumbukwe kwa mambo nane  Send to a friend
Thursday, 30 September 2010 19:45

Ibrahim Bakari, Kaliua
MGOMBEA urais kwa tiketi ya CCM, Jakaya Kikwete amesema anataka Watanzania wamkumbuke kwa mambo nane wakati atakapoondoka Ikulu 2015.

Kikwete alisema hayo alipokuwa akizungumza na wananchi kwenye Jimbo la Urambo Magharibi alipokuwa akiomba ridhaa ya wananchi kumrejesha kuongoza serikali kwa kipindi kingine cha miaka mitano.


"Nimesema kuna mengi nayafanya, lakini nikimaliza kipindi changu nataka watu wanikumbuke kwa mambo nane... waseme Mungu amrehemu, yule bwana acha tu, amefanya kitu."

Huku akishangiliwa na mashabiki, wanachama na wapenzi wa CCM, Kikwete aliyataja mambo hayo kuwa ni; kuimarisha kilimo cha umwagiliaji kupitia mpango aliouasisi wa Kilimo Kwanza, matumizi bora ya mbolea, dawa za kilimo, kutoa wataalam na maofisa wengi wa kilimo.
Pia kusaidia upatikanaji wa masoko kwa mazao ya wakulima, kusimamia uwepo wa bei bora za mazao, kuimarisha barabara ili wakulima waweze kusafirisha mazao kutoka vijijini na kuachana na jembe la mkono na kutumia matrekta makubwa na madogo.

Kikwete aliyekiri kutofikiwa malengo kwa maeneo mbalimbali katika sekta ya maji na barabara, alisema katika kipindi cha miaka mitano ijayo serikali imejipanga kikamilifu kutekeleza ahadi zake.
Alisema kuna mengi yanahitaji misaada ya wahisani ikiwa ni pamoja na ujenzi wa barabara, ujenzi wa miundombinu ya kisasa ya maji hivyo ni lazima tuwatafute wahisani.

Akizungumzia safari zake za nje, Kikwete alisema: "Wapo wanaosema nasafiri sana,  sasa ningekaa pale nyumbani kwangu nikamwangalia mke wangu Salma halafu nimwambie aisee ulivyopendeza, Watanzania wangekufa njaa na Wajapan wanaotaka kusaidia, leo hii wasingeijua Kaliua.

"Sasa kuyapata yote haya, lazima nisafiri. Nilikuwa Marekani, nikakutana na wahisani mbalimbali; wenyewe wananiuliza wanataka wanisaidie wapi, mimi nasema hapa na hapa na pale... kuna watu wanapesa nyingi tu."
Akizungumza katika mkutano huo, mbunge wa Urambo Magharibi, Prof.  Juma Kapuya alisema CCM wameshafundishana kucheza mpira wa uchaguzi.

"Pasi ya kwanza anatoa diwani, diwani kwa mbunge na mbunge anatoa kwa rais anafunga goli... Kikwete ni (mshambuliaji wa Simba, Mussa Hassan) Mgosi wa CCM, ukimpa mpira anafunga," alisema Kapuya na kuamsha vicheko kwa wote waliofika kwenye mkutano huo.

Naye Kikwete aliyekuwa pembeni, baada ya Kapuya kumaliza, alisema: "Aah! Mimi bwana na Kapuya kuna mengi tunakubaliana, lakini katika soka, tuko timu tofauti, mimi siko huko," alisema Kikwete ambaye anajulikana kama shabiki mkubwa wa Yanga wakati Kapuya ni shabiki asiyejificha wa Simba. Hata hivyo alimaliza kwa kusema: "Timu bora inajengwa na ngome imara, kiungo imara na safu yenye mtazamo mmoja na ndiyo inayoshinda kuliko kuchanganya."


Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
Reddit! Del.icio.us! Mixx! Free and Open Source Software News Google! Live! Facebook! StumbleUpon! TwitThis Joomla Free PHP
 

Comments 

 
0 #40 2010-10-06 14:55
huyu jamaa yenu hana hata aibu,,,,,,,wa lumkumbuka nadhani sio wananchi walioteseka kimaisha kwa muda wote aliokuwepo madarakani bali ni hao mafisadi anaowakingia kifua..ndo hayo tu jamani..God bless chadema
Quote
 
 
0 #39 2010-10-02 10:31
MTU MWEMA HUACHA ALAMA ZA NYAYO ILI WANAOFUATA WAONGOZWE NAZO, ILA KWENYE NYAYO ZA ZA DHALIMU, WEMA WALIOBAKI HUZIWEKEA MIIBA ILI WENGINE WASIUMIZWE!

A GOOD PERSON LEAVES FOOTPRINTS SO THAT THOSE WHO FOLLOW MAY BE LED ON THAT PATH, BUT A DESPOT'S PRINTS ARE COVERED BY THE GOOD PEOPLE WITH THORNS SO THAT OTHERS MIGHT NOT GET HURT!
Quote
 
 
0 #38 2010-10-02 06:10
EVARIST KAUKI HEBU NITUMIE HAYO MAMBO AMBAYO HUYU BRO NA CHAMA CHAKE WAMEKIFANYA, daudsafari@yaho o.com
Quote
 
 
-1 #37 2010-10-02 00:50
Mipango ni mingi lakini inategemea wahisani, kama ni hivyo kunasababu ya kujidai na hiyo mipango, maana wahisani wanatoa pesa kwa wakati wanaotaka, mara nyingi siku hizi wanataka waridhishwe na shughuli zinavyofanywa na serikali.
Japan nchi yenye eneo dogo tunaomba chakula kwao hadi lini na nikitu cha kutamba mbele za watu.
Quote
 
 
-1 #36 2010-10-01 23:44
Quoting Elton:
Haya si mambo manane, kimsingi ni jambo MOJA tu, ambalo ni KILIMO! Mengine saba tutajie , ni yepi hayo? Hilo ni jambo moja, sio nane acha kutufanya mbumbumbu, Elimu? Afya? Jamii bora? Ajira? Usimamizi bora wa rasilimali? Miundombinu bora? Uchumi imara? Uongozi na utendaji bora serikalini? Kutokomeza Rushwa? Ni nini tutakukumbukia boss??

Ni kweli kabisa.
Quote
 
 
-1 #35 2010-10-01 22:16
kati ya watu ambao hata kuwasikia natamani roho yangu itoke ni huyu mkwele wa charinze naomba cku itokee adondoke tena jukwaani apotee kabisaaa duniani.kikwete watanzania tumekuchoka muachie dr atufanyie mambo wa-Tz.naanza kufunga 3 kavu kikwete adondoke singida ili tumpoteze
Quote
 
 
-2 #34 2010-10-01 21:18
Nyie Chadema acheni porojo. Hamwezi kutawala nchi. Slaa hawezi kuwa rais. Inaelekea anayeendesha hii sehemu ya maoni anachagua maoni. Maoni yangu yanatoka mara moja moja. Halafu maoni yote ya Pro Kikwete na CCM yanatoka kwa shida sana. Mwananchi oyeee kwa kushabikia chadema na Slaa. Ama kweli mwananchi limepoteza umaarufu wake wa kuwa gazeti neutral.
Quote
 
 
+1 #33 2010-10-01 15:25
washikaji nina ombeni email adress zenu niwape mambo ambayo amefanya Kimefanya chama cha mapinduzi katika picha. tumia email adress hii evaristkauki@ya hoo.com
Quote
 
 
+2 #32 2010-10-01 15:24
mkwele ungejua unavyonikera na hilo neno wahisani, acha tu
Quote
 
 
+1 #31 2010-10-01 14:58
Quoting Administrator:
Quoting dina mbiwayo:
UNACHELEWA SANA KUPOST MAONI YA KIKWETE MI NIMEKUWA NAKUANGALIA TU ADMIN

Hayo sio ya kweli.

Quoting Administrator:
Quoting dina mbiwayo:
UNACHELEWA SANA KUPOST MAONI YA KIKWETE MI NIMEKUWA NAKUANGALIA TU ADMIN

Hayo sio ya kweli.
Quote
 
 
+1 #30 2010-10-01 14:46
mbona maoni yangu hayawekwi?
Quote
 
 
+5 #29 2010-10-01 14:45
Ungukuwa na akili Kikwete ungeachia wenzako ukatulia ungejijengea heshima kubwa mno katika nchi na kimataifa. Lakini kwa kuwa undanganywa sana utajiabisha sana nchi imeshakushinda mheshimiwa salimu amri achie wengine wajaribu ili kukuza demokrasia. Ninaumia sana na mambo unayoahidi kama umekatwa kichwa. Inaonyesha ni jinsi gani ulivyokulia kijeweni na uswahili mwingi. Mambo ya nchi hayahitaji mambo ya kijiweni nafikiri na ninadhani huwa hufikirii kabla ya kuongea na kupanga hoja. Tetea taaluma yako uliyotunukiwa walao kwa matendo. Waache wenye kudhubutu wafanye mabadiliko halafu ndio uje uombe tena utakuwa umejifunza ulipokosea. Kuliko sasa hutaiweza kabisa wapishe wakusaidie kurudisha heshima ya nchi.
Quote
 
 
+5 #28 2010-10-01 14:42
ok,jk ni mtu wa watu ndiyo ila asitumie iyo nafasi kuhadaa umma
Quote
 
 
0 #27 2010-10-01 14:31
sasa ni muda upi wa kuyaweka hayo maoni?
Quote
 
 
-1 #26 2010-10-01 14:29
siweki maoni kwani tokea nimeanza kuweka maoni, sijaona wayaweke !
Quote
 

Add comment

Tumia jukwaa ili kutoa maoni ambayo yatasaidia kulijenga taifa letu. Kumbuka, maoni yako yatapitiwa kwanza kabla hayajarushwa hewani!!!!!!


Banner
Banner
Banner