MwanzoContactsEmail
Home Habari Uchumi na Biashara Rostam aponda tiba ya Mchungaji Loliondo
BOOKMARK THIS PAGE
Rostam aponda tiba ya Mchungaji Loliondo  Send to a friend
Tuesday, 15 March 2011 21:22

Shija Felician, Igunga
WAKATI Watanzania wengi wakimiminika kwenda wilayani Loliondo, mkoani Arusha kupata dawa inayodaiwa kutibu magonjwa sugu, Mbunge wa Igunga (CCM), Rostam Aziz ameibuka na kusema tiba hiyo haina lolote akidai kwamba ndugu zake watano wameitumia lakini hawajapona.

Akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara wa kuwashukuru wapigakura uliofanyika kwenye Viwanja vya CCM wilayani Igunga, Tabora mbunge huyo alisema haiamini dawa hiyo kwa kuwa ana ushahidi kwa ndugu zake hao ambao anadai kwamba wanaendelea kuugua kisukari licha ya kutumia dawa hiyo siku saba zilizopita.

Aliwataka wale watakaokwenda Loliondo ambao wanatumia dawa za hospitalini kuendelea kuzitumia badala ya kuzipuuza na kuzitupa... “Ndugu zangu wananchi wa Igunga, mimi mjomba wangu Hassan mnamfahamu karibu wote hapa mjini ni mgonjwa wa siku nyingi wa kisukari. Ameshakunywa dawa hiyo lakini mpaka sasa ni mgonjwa kama mnavyomuona sasa hiyo dawa inaponyesha nani?”

Hata hivyo, aliwataka wananchi wote wenye imani juu ya dawa hiyo waende huku akiwasisitizia kutopuuza ushauri wa madaktari kwani.

Wakati Rostam akipinga dawa hiyo, wilayani Kahama, mamia ya wafanyabiashara wamefunga shughuli zao na kukimbilia Loliondo kwa Mchungaji Mwasapile kunywa dawa hiyo huku baadhi ya waliorejea baada ya kuinywa wakidai kuwa hali zao sasa ni nzuri.

Wafanyabiashara hao wengi wao wanaondoka kwa siri wakidai wanakwenda Dar es Salaam katika shughuli zao, lakini siri imefichuka baada ya baadhi yao kuoneka katika runinga wakiwa katika foleni wakisubiri kupatiwa huduma hiyo.

Mbali ya kuzungumzia suala hilo la tiba ambalo limegusa hisia za wananchi wengi wa Afrika Mashariki, mbunge huyo aliwapa pole wananchi wa Igunga ambao nyumba zao zimeezuliwa na upepo uliosababishwa na mvua kubwa zilizonyesha wiki iliyopita ambazo ziliathiri kaya 19. Aitoa msaada wa Sh500,000 kwa kila kaya iliyokumbwa na maafa hayo.

Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
Reddit! Del.icio.us! Mixx! Free and Open Source Software News Google! Live! Facebook! StumbleUpon! TwitThis Joomla Free PHP
 

Comments 

 
0 #52 2011-03-18 18:21
we Rostam, ni mtu wa ajabu sana! unaongea hayo uyasemayo, kama nani? waziri wa afya? Hebu tuondokee huko na ufisadi wako huku ukishindwa kujenga hata nyumba nzuri pale Mwisi ulipozaliwa! Nduguzo hawakupona kwa kutumia dawa ya 'babu' kutokana na matendo yako maovu kwa watanzania! Mbona bungeni, huongei kitu, unasinzia tu!
Quote
 
 
0 #51 2011-03-17 05:41
wewe rostam hebu tuondolee ujnga wako hapa umeeambiwa lazima uwe na imani utapona wewe na mjomba wako mkitaka kupona rudisheni mali za watanzania mlizoiba.huna adabu
Quote
 
 
+2 #50 2011-03-16 18:05
wewe unacheza kiduku rostam. dili la dowans likitiki hupandi jukwaani. ingekuwa ni mwingira na rostam wangeoteshwa ya mwasapile watanzania wangejuta. mwingira angesema dawa hiyo itauzwa kwa fedha sawa na kununua kanisa la uhakika zaidi ya la kakobe. mwingira angemtaja huyo yesu kwa zaidi ya mara nyingi isiyohesabika halafu angetibu tu wakanisa lake kwa ubaguzi. ndio maana mungu alimpa ndoto hizo mtu asiye na tamaa. ingekuwa ni rostam amepewa ndoto hizi angeuza dawa hiyo kwa kila mtanzania bilioni moja moja ili angalau awanunulie wale watoto magari me[NENO BAYA] zaidi. alaaniwe mtu yule ambaye kwa nia mbaya zake anawadhulumu masikini. haponi mtu huyo wala jamaa yake wala chochote kinachomfaa yeye.
Quote
 
 
+2 #49 2011-03-16 17:45
mwingira ni mchungaji? anamchunga nani?
rostam kama umesoma masharti manne ya babu utajua kwa nini hukupona na kwa nini hutapona. moja dawa ya babu si sindano ya kudunga ya masaa wala siku saba. dawa ya babu ni IMANI na ukiwa na imani utapona. halafu dawa ya babu ni kwa wasio na usanii kwa watanzania. wapo naweza kukutajia ukitaka ambao babu aliwaambia wakatubu dhambi zao halafu warudi ili awape dawa. labda hakukusemea lolote kwa sababu za usalama wake. ila elewa tu dawa ya babu ni uponyaji kwa imani. kwani ulimpeleka huyo mjomba kwa kakobe? kwa nini? MPELEKE HUYO MGONJWA WAKO KWA MWINGIRA NIMEOTESHWA NI TABIBU WA WAGONJWA WAKO.
Quote
 
 
0 #48 2011-03-16 16:15
Mwingira, kanisa la Efata lilianzishwa kwa wizi wa sadaka kama anavyo iba yeye na kununua gari mnamo mwaka 1971, kwa ajili ya VIZIWI (Deaf Missionary na mwanzilishi alikuwa kiziwi akiitwa VERMON MILLER Akitokea Metro huko Lima kwenye municipality ya VILLA EL SALVADOR, chini ya kanisa la Seventh Day Adventist. Wewe ukaona sasa uanzishe wizi wako. Utukome, umkome Babu, na uwakome watanzania wote. Toa boriti lako kwenye jicho ndipo utaona lile la BABU mtoa dawa. [NENO BAYA] mkubwa wewe.
Quote
 
 
+1 #47 2011-03-16 16:07
Rostam, wewe tukikuona gizani tutakuua kwa kutuletea maisha magumu, funga domo lako [NENO BAYA] wewe. Mwizi mkubwa, ongea ya dowans na siyo ya dawa. huna adabu.
Quote
 
 
+1 #46 2011-03-16 14:35
Acha kupotezea mkuu, tutakuona wa maana utakapozungumzi a shutuma zinazokuhusu. Bungeni hujawahi kuongea na shutuma hujawahi kujibu. Unakimbilia kumshambulia Babu wa watu kama alikukosea kitu. Aliwalazimisha hao ndugu zako waende? Unaanza kubwata sababu ushatafu[NENO BAYA] soko la hiyo mitambo ya DOWANS na dalali wako Makamba (Mbunge) ambayo ingebidi serikali uliyoiweka mikononi kwako iitaifishe mitambo yako. TUNATAKA UJIBU SHUTUMA ZAKO NA KUWAJIBIKA IKIBIDI.
Quote
 
 
+5 #45 2011-03-16 14:29
mimi ningeshangaa sana kama hao ndugu zako wangepona mtoto wa nyoka ni nyoka mtu kama wewe shukuru unaishi kwenye nchi inayo ongozwa kishikaji ingekuwa nchi nyingine ungekuwa umeshanyongwa siku nyingi.
Quote
 
 
+2 #44 2011-03-16 14:13
Hakuna fisadi atakayepona kwa dawa ya babu, hata huyo rafiki yako wa nyanda za juu haitamsaidia kitu.
Quote
 
 
+5 #43 2011-03-16 14:05
sasa wewe unadhani unapofanya mazambi ndugu zako nao si wanakuombea uendelee kuwa fisadi, sasa wtaponaje? wewe na ndugu zako wote wazambi, kwanza ningeshangaa kama wamepona.
Quote
 
 
+2 #42 2011-03-16 13:54
rostam umeyataka mwenyewe, kwenye mambo ya dowans ulinyamaza lakini maswala yanayosaidia jamii unatafuta nanma ya kuyadidimiza tukueleweje wewe? unaitakia nini nchi hii? jieleze kwa watu ulishirikiana na nani kufanya ufisadi baaaaaasi lakini maswala mengine ya nchi yetu hayakuhusu. acha watu wanywe hata mavi kama wanapona.
Quote
 
 
+4 #41 2011-03-16 13:46
Pengine unaogopa kuombwa msaada wa kuwapeleka wapiga kura wako huko kwa Babu ukaona bora uanze na kumkandia huyo Babu wa watu?

Au unaogopa maneno ya Mzee Ndesa wa kuwahimiza wabunge wawasaidie wapiga kura wao kufika kwa Babu?

Mbona rafiki yako wa Monduli amesema dawa ya Babu ni safi?

Hiloooooooo!!!! !!!
Quote
 
 
0 #40 2011-03-16 13:46
It is because of poor medical goods and services. goods in terms of medicene(fake), hospitals,dispe nsaries and health centers very few, unreachableand services in terms of quality eg the service is not prompt doctors and nurses are not easily accessible,not committed /motivated,they are not performing duties with care diligence and intergrityso until and unless the state curbs the above espesially fake medicine civilians will continue flocking/flowing to Babu.The state is duty bound for their security .
Quote
 
 
+1 #39 2011-03-16 13:34
Quoting mchunga k:
Rostam alikuwa anaongea na wapiga kura wake. tuwaache wao wamshambulie. jojas kinakuuma nini? mbona wana igunga wamemuelewa? kwa baba nenda wewe hajakukataza. hata watu wake hajawakataza."Hata hivyo, aliwataka wananchi wote wenye imani juu ya dawa hiyo waende huku akiwasisitizia kutopuuza ushauri wa madaktari kwani". wewe unasoma habari nusu nusu. kichwa cha panzi



Babu alishaonya kuhusu tabia na mienendo yetu kuhusiana na dawa yake. Hao ndugu wa Rostam unategemea 500 zao wamezitoa wapi kama sio kwenye mafungu ya dhuluma ya richmond na dowans. Hela yao haijaswii, kamwe hawawezi kupona. wakitaka kupona, waende mtaani wakafagie barabara, walipwe hela halali kwa kadiri ya jasho lao, then waende tena Loliondo kwa babu na hela hiyo halali, wasipopona basi wana laana ya milele. Adumu Mchngj Ambikile na tiba yake isiyopenda mafisadi
Quote
 
 
0 #38 2011-03-16 13:29
Quoting sikitiko kijaa:
Soma hii kwa makini kama una akili. kama huna "kalaga baho na ubozi wako". Josephat Mwingira wa Kanisa la Efatha amemuombea mabaya Mchungaji Ambikile Mwasapile anayetoa tiba ya magonjwa sugu katika kwamba anapaswa kulaaniwa hadi kufa kutokana na kutoa huduma hiyo.

Mwingira alisema “Hizi ni roho za kishetani zinazotaka kuwaangusha walio wengi ambao hawamjui Yesu Kristo kwani haiwezekani mtu atumiwe na Mungu halafu hata siku moja asimtaje Yesu. Asitumie Biblia hata kuwahubiria watu wamtumaini muumba wao,”alisema Mwingira.

Mwingira alisema huduma hiyo ni uongo na kwamba haina tofauti na Deci iliyokuja kiujanja ujanja na kuteka watu wengi baadaye walijutia maamuzi yao. “Kama mpakwa mafuta wa Bwana niliyeitwa kwa kusudi lake. Nailaani Loliondo ife pamoja na Mchungaji wake na itoweke kama Deci ilivyotoweka

Alisema kama alivyoilaani Deci na ikafa, anailaani huduma ya Loliondo ili ife kwa kuwa mchungaji huyo ni roho ipotezayo, inayotaka kuwateka watu walioko gizani na kuwaangamiza.
“Sitakubali kuendelea kuona roho hiyo ikipoteza watu. Nailaani itoweke Loliondo na iangamie kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareti,”alisi sitiza. Mwingira alisema haiwezekani kwa mtu aliyeitwa na Mungu kuwahudumia watu wake, baadhi ya watu hao wafe kwenye huduma yake.

“Ni wagonjwa wangapi wamepelekwa kule na wengine wamefariki nyumbani kwake kabisa na wengine njiani, je mlishawahi kujiuliza? alihoji Mwingira.

Hii nayo ipo katika gazeti hili hili



Mwingira nae ana hofu mishemishe zake zitaanguka. Tuwe makini na watu wanaoishi kwa kutegemea sadaka. siku zote wasiwasi wao ni kupoteza wafuasi ambao ndio chanzo cha mapato na migari heavy wanayotembelea.
Quote
 

Add comment

Tumia jukwaa ili kutoa maoni ambayo yatasaidia kulijenga taifa letu. Kumbuka, maoni yako yatapitiwa kwanza kabla hayajarushwa hewani!!!!!!


Banner
Banner
Banner