Burudani
Makala
Habari nyingine
Hadithi
Kolamu
Maoni ya wasomaji
Habari na Picha
Nafasi za kazi
Kona ya Marafiki
 
 
 
Date::10/17/2009
Rais Kikwete kukabidhiwa Kombe la Dunia Novemba Dar
Mshambuliaji wa Yanga,Mike Barasa na mlinzi wa Azam, UIbrahim Mwaipopo wakiwania mpira mjini Dar es Salaam jana ambapo timu hizo zilitoka sare 1-1.
Na Ibrahim Bakari

RAIS Jakaya Kikwete atakabidhiwa Kombe la Dunia siku moja baada ya kuwasili jijini Dar es Salaam.

Kombe la Dunia linalozunguka mataifa mbalimbali ya Afrika, litawasili nchini Novemba 19 likitokea Addis Ababa, Ethiopia na litakuwa nchini kwa siku tatu.

Akizungumza katika mahojiano maalum na Mwananchi Jumapili juu ya hatua iliyofikiwa ya maandalizi ya ujuo wa kombe hilo, Meneja wa Coca-Cola Tanzania, Heriette Mutayoba alisema kuwa taratibu zinaandaliwa ili rais atoe salaam zake.

"Tunapanga iwe hivyo, lakini bado taratibu zinaandaliwa. Nchi nyingi tunaona marais wametoa salaam zao kama Ghana, Liberia na kwingineko, sasa taratibu zinaandaliwa na rais wetu aseme neno lake.

"Tunapanga Novemba 20, lakini hatujajua ratiba yake itakuwa vipi kama siku hiyo hiyo likiwasili vyote tutajua na tutatoa taarifa kamili," alisema Mutayoba.

Rais Kikwete alilipokea kombe hilo lilipowasili Januari 15 kwenye Hoteli ya Movenpick na kutangaza mikakati mbalimbali ya maendeleo ya soka ikiwemo kumleta kocha wa timu ya taifa, Taifa Stars.

Akizungumzia maandalizi ikiwa zimesalia siku 30 kabla ya kombe kuwasili nchini, Mutayoba alisema kampuni yake imejipanga tayari kwa mapokezi hayo.

"Kwanza tunaandaa utaratibu, kombe litakapowasili, tungependa mashabiki waje uwanja wa ndege kulilaki na walione, na kisha tutawapa siku yao, Novemba 21 kuanzia asubuhi mpaka saa 12 jioni kulishuhudia kwenye Uwanja wa Taifa," alisema.

Alisema taratibu za kuchezwa mechi iwe ya klabu ama timu ya taifa zinaandaliwa na mambo yakikamilika yatakuwa hadharani.

Aliwataka mashabiki kujitokeza kwa wingi lakini akasisitiza kuwa itapendeza kama kila mmoja atajitokeza kwa amani na utulivu bila kufanya ghasia.

Aliwataka wadau wa soka nchini kulichukua Kombe la Dunia kama sehemu ya changamoto ya timu zao kufanya vizuri katika mashindano mbalimbali pamoja na kutoa hamasa kwa timu ya taifa.

Facebook
        Contact Us DISCLAMER
Email:webmaster@mwananchi.co.tz © Mwananchi Communications Ltd 2006-