UKAME MVOMERO: Mfugaji Penet Marko akionyesha baadhi ya ng’ombe waliokufa katika kitongoji cha Ranchi-Sokoine, kijiji cha Wami-Sokoine Wilaya ya Mvomero. Katika kitongoji hicho ng’ombe zaidi ya 2,700 wamekufa katika kipindi cha miezi mitatu wakati wilaya nzima ya Mvomero kwa mujibu wa Kaimu Katibu Mkuu wa Chama Cha Wafugaji Tanzania, Joshua Lugaso, ng’ombe waliokufa kutokana na ukosefu wa malisho na maji ni 17,000. Picha zote na Juma Mtanda