Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Feza Boys wakiwa wamembeba Alfred Shauri aliyeshika nafasi ya kwanza katika matokeo ya mtihani wa kidato cha nne yaliyotangazwa na Baraza la Mitihani la Taifa, jijini Dar es Salaam jana. Picha na Said Khamis
Photo: 1/9
Wanafunzi wa kidato cha nne wa Shule ya Sekondari ya Kidete iliyopo wilayani Kigamboni mkoani Dar es Salaam. Shule hii ndiyo iliyoshika nafasi ya mwisho katika matokeo ya kidato cha nne mwaka 2016 yaliyotangazwa jana . Picha na Ericky Boniphace
Photo: 2/9
Wachuuzi wa Mafenesi wakiyaanda kwa kuweka katika vifungashio maalum kabla ya kuyauza kwa wateja katika mtaa wa Azikiwe jijini Dar es Salaam. Picha na Said Khamis
Photo: 3/9
KIAPO: Mbunge wa Kuteuliwa, Profesa Palamagamba Kabudi akila kiapo cha utii bungeni mjini Dodoma jana. Picha na Emmanuel Herman
Photo: 4/9
BIASHARA: Mfanyabiashara wa samaki katika Soko Kuu la Bukoba mkoani Kagera, Enock Onesmo (kushoto) akimuonyesha mteja wake, Ayoub Abdallah kitoweo aina ya hongwe aliyekuwa akimuuza kwa Sh20,000. Picha na Phinias Bashaya
Photo: 5/9
KERO: Mludikano wa uchafu uliochanganyika na tope umekuwa kero kwa wachuuzi na wateja katika Soko la Buguruni jijini Dar es Salaam. Picha na Ericky Boniphace
Photo: 6/9
Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania, Dk Charles Msonde akitangaza matokeo ya mtihani wa kidato cha nne wa mwaka 2016, jijini Dar es Salaam jana. Picha na Said Khamis
Photo: 7/9
Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Chohero iliyopo halmashuari ya Mvomero mkoani Morogoro, wakicheza nje ya madarasa ya shule hiyo wakati wa likizo mwishoni mwa Desemba mwaka jana. Picha zote na Nuzulack Dausen.
Photo: 8/9
Rais John Magufuli akisalimiana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Antonio Guterres kabla ya kuanza mazungumzo yao katika Ofisi za Makao Makuu ya Umoja wa Afrika (AU), yaliyopo Addis Ababa nchini Ethiopia, jana. Picha na Ikulu