
| Kwa upotoshaji huu, Ismail Jussa aombe radhi | Send to a friend |
| Wednesday, 25 January 2012 20:53 |
LEO tumechapisha habari zinazomnukuu Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka akishangazwa na kauli iliyotolewa katika Baraza la Wawakilishi na Mwakilishi wa Mji Mkongwe kwa tiketi ya CUF, Ismail Jussa kwamba andiko lililowakilishwa katika Umoja wa Mataifa (UN) na waziri huyo kuomba eneo la ziada nje ya maili 200 za Ukanda wa Kiuchumi Baharini (EEZ) halikufanywa kwa niaba ya Serikali ya Muungano kwa madai kwamba Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) haikushirikishwa. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Waziri Tibaijuka alisema andiko hilo liliwasilishwa Januari 18 mwaka huu kama ombi la Serikali ya Jamhuri ya Muungano na kuongeza kuwa, SMZ ilishirikishwa kikamilifu tangu mchakato wa kuandaa mradi huo ulipoanza mwaka 2007. Waziri alitoa kauli hiyo baada ya mwakilishi huyo kuwasilisha hoja binafsi katika Baraza la Wawakilishi mwanzoni mwa wiki, akilitaka Baraza kutolitambua andiko hilo lililowasilishwa UN na kuliomba liiagize SMZ kutojihusisha na mpango huo kwa namna yoyote kwa madai kwamba ni mpango wa kuhujumu eneo la bahari la Zanzibar. Mwakilishi huyo alikwenda mbele zaidi na kumtaka Waziri wa Ardhi, Ali Juma Shamhuna ajiuzulu, vinginevyo awajibishwe na Rais, huku akiungwa mkono na wajumbe waliosimama kuchangia hoja hiyo. Tunampongeza Waziri Tibaijuka kwa uamuzi wake wa kukutana na waandishi wa habari jana na kuchukua muda mrefu kutoa ufafanuzi wa suala hilo ambalo tunadhani lingeweza kusababisha msuguano usiokuwa wa lazima kati ya pande mbili hizi za Muungano wetu. Tunasema hivyo kwa sababu tuhuma alizotoa mwakilishi huyo ni nzito mno pengine kuliko yeye anavyofahamu. Ndiyo maana tuhuma kama hizo zinapotolewa, serikali makini popote duniani hulazimika kuzijibu kwa ufasaha pasipo kuzibeza au kutoa majibu ya mkato kwa nia ya kuzificha chini ya zulia. Hivyo ndivyo Waziri Tibaijuka alivyofanya na tunakubaliana naye kabisa aliposema alilazimika kutoa ufafanuzi wa kina kwa sababu pande hizo mbili za Muungano hazipaswi kugombea fito wakati nyumba inayojengwa ni ya wote. Moja ya sababu zinazotufanya turidhishwe na ufafanuzi wake ni pale alipotoa ushahidi wa namna Zanzibar ilivyohusishwa kikamilifu kupitia SMZ katika ngazi zote tangu 2007, kiasi cha kuibua mashaka kama kweli mwakilishi huyo wa Mji Mkongwe alipeleka hoja hiyo barazani kwa nia njema au alidhamiria kuwachafua viongozi wa pande hizo mbili za Muungano kwa kupeleka hoja iliyojengwa kwa misingi ya maneno ya mitaani? Ufafanuzi wa Waziri Tibaijuka umetufumbua macho na sasa tumeelewa kwamba mchakato huo mkubwa na muhimu uliendeshwa na kamati mbalimbali zilizoundwa tangu mwaka 2007, ikiwamo kamati ya makatibu wakuu iliyoongozwa na Katibu Mkuu katika Wizara ya Maji, Nishati, Ujenzi na Makazi Zanzibar, Mwalimu Mwalimu na kwamba aliyekuwa Mkurugenzi wa Upimaji Ramani, Haji Adam Haji ndiye aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi. Sasa tumejua pia kwamba Pandu Makame kutoka katika Ofisi ya Makamu wa Rais ndiye aliyeteuliwa kuwa mwenyekiti mwenza wa Kamati ya Utekelezaji. Tumefarijika kusikia kutoka kwa waziri huyo kuwa, zoezi la kupima alama za sehemu ya bahari inayoombwa lililofanyika Januari mwaka jana, masheha wa Kiuyu, Maziwa Ng’ombe, Kojani na Vitongoji walioko katika Kisiwa cha Pemba walishirikishwa, huku wenzao wa Makunduchi katika kisiwa cha Unguja pia wakishirikishwa. Hata wakati wa kuwakilisha andiko hilo huko UN ujumbe wa nchi yetu uliwahusisha viongozi wa pande mbili za Muungano, akiwamo Mkurugenzi wa Sera na Mipango, Ayoub Mohamed Mahamoud. Sisi wa Mwananchi tunajivunia rekodi yetu ya muda mrefu ya kutetea haki za wananchi wa Zanzibar pale tunapoona zinakiukwa. Lakini tumefadhaishwa na tuhuma hizo zilizotolewa dhidi ya SMZ na Serikali ya Muungano na mwakilishi huyo wa Mji Mkongwe. Tunamshauri apate ujasiri na kuomba radhi kwa Baraza la Wawakilishi, SMZ na Serikali ya Muungano kwa upotoshaji mkubwa alioufanya. |



LEO tumechapisha habari zinazomnukuu Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka akishangazwa na kauli iliyotolewa katika Baraza la Wawakilishi na Mwakilishi wa Mji Mkongwe kwa tiketi ya CUF, Ismail Jussa kwamba andiko lililowakilishwa katika Umoja wa Mataifa (UN) na waziri huyo kuomba eneo la ziada nje ya maili 200 za Ukanda wa Kiuchumi Baharini (EEZ) halikufanywa kwa niaba ya Serikali ya Muungano kwa madai kwamba Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) haikushirikishwa. 











Comments
HALAFU NI LINI MUTATURUHUSU NA SISI KUTOKA ZNZ KUJA KUPIMA MAENEO YA TANZANITE NA LAMASI HUKO BARA?....MUSIJALI TUTAWASHIRIKISH A WATU 2 MPAKA 3, WAJUMBE WA NYUMBA 10.!!!!
Mh. Tibaijuka amepuuza azimio la BLW lilionesha mipaka ya ZNZ na na kuondosha mafuta katika mambo ya muungano. Hii inoanesha dhahiri ni jinsi gani serikali ya muungano haijali kuwepo kwa serikali ya ZNZ. na maamuzii yake.
Ikizinga[NENO BAYA] kua UCHUMI SI SULA LA MUUNGANO!!!!
Tibaijuka unataka kukuza uchumi upi?!!!
Ikiwa hivi...nani ataumia!???
Na kwa hilo Watanganyika hamtowahi kutuzunguka.
Jussa Hongera sana.
Kuna watu wengine ni ma-p-unguani kweli.Hivi unadhani Watanganyika wanafadika na huu muungano?wazanzibari ndo tumukuwa tukiwabeba kweli.Mpaka bili za umeme tunawalipia.Muungano ukivunjika itakuwa poa tu manake nadhani wapemba wote wataondoka Kariakoo.iNFACT HATA SS HATUWAPENDI HATA KIDOGO.TUMECHOKA KUBEBA WATU WASIO NA SHUKURANI.
Hivi ndio Tanzania mbili zilivyotambulis hwa. Ya kwanza ni January 2007 kwenye mambo ya mazingira na ya Pili ni January 2012 Kulaghai kupata upenu wa Zanzibar na mafuta. Ulghai wa hali ya juu huu.
I – Ya mazingira - January 2007
-----------
1. 0 INTRODUCTION & SETTING
1.1. Country Background
The United Republic of Tanzania is the largest country in the East Africa. It is located between 1 degrees
South and 12 degrees South latitude and 30 degrees East and 40 degrees east. It is constituted by
Mainland Tanzania and Tanzania Zanzibar. It is a vast country with a total area of 945,087 Sq. km
comprised of land area of 883,749 sq. km (881,289sq.km mainland and 2,460sq.km Zanzibar), plus
59,050 sq. km inland water bodies (URT, 2002a). It shares borders with eight countries. Its neighbours
include Kenya and Uganda in the North, Rwanda, Burundi and Democratic Republic of Congo in the
West, Zambia and Malawi in the South West and Mozambique in the South. [Figure 1`- Political Map of
Tanzania] Mainland Tanzania borders the main water bodies of Africa. To the east is the Indian Ocean, to
the north Lake Victoria, to the west Lake Tanganyika and to the south-west Lake Nyasa. Mainland
Tanzania also has the highest point in Africa. The snow caped Mount Kilimanjaro is 5,950 metres high.
Based on the 2002 Population and Housing Census, the country was reported to have about 34,569, 232
people: 33,584,607 from mainland Tanzania and 984,625 from Zanzibar with an annual average
intercensal growth rate (1988 – 2002) of 2.9 (URT, 2002b). By 2005 the country has about 36.2 million
people (17.7 million people were males and 18.5 million people were females).
--------------------------------------------
II – Ya Mafuta - January 2012.
==========================
2. 1.2 Tanzania is an independent, sovereign, coastal State located in the Eastern Africa region. It is bound between latitudes 1° 00’ and 11° 45’ south of the Equator and longitudes 29° 15’ and 41° 00’ east of the Greenwich meridian. Tanzania is bordered by the Republics of Kenya and Uganda to the north, Rwanda and Burundi to the northwest, Democratic Republic of Congo to the west, Republic of Zambia to the southwest, Republic of Malawi and the Republic of Mozambique to the south. Tanzania also shares the waters of the Indian Ocean with the Republics of the Seychelles and Comoros to the east and southeast, respectively.
1.3 Tanzania has an estimated population of 44,485,0002 and covers a total area of 948,740 square kilometers with land covering approximately 889,460 square kilometers. The coastline of Tanzania extends approximately 1,400 km in a north-south direction from the Tanzania-Kenya border to the Tanzania-Mozambique border to the south.
Jee unadhani haya yalifanyika kimakosa?
Source UN.