MwanzoContactsEmail
Home Uchambuzi Maoni ya Mhariri Ukimya wa Serikali afya ya Dk Mwakyembe ni aibu
BOOKMARK THIS PAGE
Ukimya wa Serikali afya ya Dk Mwakyembe ni aibu  Send to a friend
Tuesday, 31 January 2012 21:55

HATIMAYE Naibu Waziri wa Ujenzi ambaye pia ni Mbunge wa KyeLa, Dk Harrison Mwakyembe amejitokeza na kutoa kauli nzito kuhusu chanzo cha maradhi yanayomsibu, huku Serikali ikiendelea kukaa kimya hata baada ya washirika wake wa karibu  kusisitiza kwamba alipewa sumu.
   
Itakumbukwa kwamba, Desemba 10 mwaka jana, Dk Mwakyembe akiwa na hali mbaya alipelekwa katika Hospitali ya Appolo, nchini India kwa matibabu baada ya kuugua maradhi yaliyosababisha ngozi yake kuharibika. Tangu arejee mwanzoni mwa mwezi uliopita alikuwa hajaonekana hadharani, mbali na kutoa tamko kwamba afya yake ilikuwa inaendelea vizuri.
   
Hata hivyo, muda wote huo aliokuwa nchini India na baada ya kurudi nchini, mazungumzo ya watu maofisini, nyumbani, mitaani na vijiweni yalitawaliwa na utata wa suala la afya ya Dk Mwakyembe, huku uvumi, tetesi na minong’ono kwamba maradhi yake yalisababishwa na hujuma za kisiasa vikitawala hisia za wananchi. Hisia hizo zilikuzwa na kauli ya mmoja wa washirika wake kisiasa, Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samwel Sitta ambaye alimtembelea hospitalini nchini India na baadaye kukiambia kituo kimoja cha televisheni hapa nchini kwamba Dk Mwakyembe alikuwa amelishwa sumu kutokana na msimamo wake dhidi ya mafisadi.
   
Akizungumza huku akionyesha kujiamini, Waziri Sitta alisema muda wote aliokaa na naibu waziri huyo katika Hospitali ya Appolo alipata ushahidi wa kutosha kwamba maradhi yake ya kuharibika kwa ngozi ya mwili wake yalisababishwa na kulishwa sumu, huku ushuhuda wake ukiacha kitendawili cha nani hasa waliohusika na uhalifu huo pasipo kuteguliwa. Hata hivyo, kauli hiyo ya Waziri Sitta iliwaudhi viongozi wengi serikalini na katika chama chake cha CCM ambao walimtaka athibitishe tuhuma kwamba hujuma kwa Dk Mwakyembe ilikuwa ni kazi ya mafisadi.
   
Lakini jambo la kushangaza ni kwamba muda wote huo Serikali ilikataa kutoa tamko siyo tu kuhusu maradhi yanayomsumbua kiongozi huyo, bali pia kama ilikuwa imefanya upelelezi kuhusu kuwapo au kutokuwapo watuhumiwa wowote ambao walikuwa wanahusishwa na hujuma hiyo. Wananchi walishangazwa na hatua ya Serikali kuendelea kukaa kimya na kupiga danadana suala hilo, huku viongozi wa Wizara ya Mambo ya Ndani na Wizara ya Afya wakitupiana mpira.
   
Tunashangazwa na ukimya huu wa Serikali hata baada ya kupata ripoti ya madaktari wa Hospitali ya Appolo ambao walimtibu Dk Mwakyembe. Haki ya wananchi kujua maradhi yanayomsibu inapewa uzito na ukweli kwamba yeye siyo tu mbunge wa kuchaguliwa na wananchi,  bali pia ni naibu waziri  katika Serikali ya Awamu ya Nne. Tukitilia maanani kwamba gharama kubwa za matibabu yake zimelipwa kwa kodi za wananchi, ndipo tunaposhangaa kwa nini Serikali haioni uhalali wa wananchi kujua hali ya afya za viongozi wao kwa madai kwamba masuala ya afya zao ni masuala binafsi.
   
Alipojitokeza hadharani mwishoni mwa wiki akiwa na washirika wake wa kisiasa katika uzinduzi wa programu ya moja ya madhehebu ya Kikristo jijini Dar es Salaam, Dk Mwakyembe aliwaeleza waumini jinsi maradhi yake ilikuwa kazi ya mafisadi ambao walimsababishia mateso makubwa na kuahidi kuzungumzia suala hilo kwa undani katika siku za usoni, huku Waziri Samwel Sitta akisimama na kuwaeleza waumini kwamba Dk Mwakyembe alilishwa sumu.
   
Sisi tunadhani ukimya huu wa Serikali umeiletea aibu kubwa na kuibua hisia kwamba, pengine nayo ni sehemu ya tatizo. Vinginevyo haiingii akilini jinsi Serikali siyo tu inavyoweza kupata ujasiri wa kuficha ripoti iliyotolewa na Hospitali ya Appolo, bali pia kushindwa angalao kutoa tamko kama Dk Mwakyembe alilishwa sumu au la.
   
Kwa kuwa Dk Mwakyembe anajua fika nini kilichomo katika ripoti iliyotolewa na hospitali hiyo ya nchini India, tunamshauri ajitokeze hadharani awaeleze wananchi ukweli kwa lengo la kumaliza uvumi, tetesi na minong’ono kuhusu maradhi yanayomsibu.
   

Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
Reddit! Del.icio.us! Mixx! Free and Open Source Software News Google! Live! Facebook! StumbleUpon! TwitThis Joomla Free PHP
 

Comments 

 
0 #12 2012-02-07 12:25
Acheni kuitetea serikali. Ripoti yote ya ugonjwa wa Dr. Mwakyembe ilishatumwa serikalini.Lakini swali ni kuwa kwa nini serikali imekaa kimya.Na kama swala lilishafikishwa hadi polisi hivyo mjue wanauhakika kuwa amepewa sumu.Ndio maana Sita ameamua kusema ukweli baada ya serikali kukaa kimya.
Quote
 
 
0 #11 2012-02-07 03:15
Mambo ya afya ya mtu ni siri ya mtu na daktari wake. Kwa mfano kama wewe ungekuwa na ngoma ungetaka mwajiri wako atoe taarifa hizo kwa umma au uzitoe mwenyewe?
Kama watu wanataka kujua kinachomsumbua Dk Mwakyembe, wamuulize Dk Mwakyembe.
Pole Dokta, tupo pamoja.
Quote
 
 
0 #10 2012-02-06 21:40
Kila jambo Lina mwisho wake
Quote
 
 
0 #9 2012-02-06 21:38
Ipo siku kila lililo la siri litajulikana
Quote
 
 
+1 #8 2012-02-03 15:08
Serikali iwe makini na kuangalia afya ya watendaji wake. Dr. Mwakyembe ni kiongozi mahiri asiyeogopa mtu anayewajali wananchi wake na Taifa kwa ujumla.

Jamani tuwe na huruma, tunapobahatika kupata kiongozi anayetujali tumtunze kama yai sio kumuangamiza tubaki na watu wasiotujali.

Mungu atamsaidia ili aendelee kututetea
Quote
 
 
+1 #7 2012-02-02 13:09
Pole sana Dr.Mwakyembe ,tunaomba usife moyo katika kututetea sisi wanyonge.
Quote
 
 
-1 #6 2012-02-01 19:21
Samweli Sitta aache kutubabaisha! Kama anajuwa [NENO BAYA] ake kalishwa sumu, kwanni asiwaseme waliofanya hivyo? Ana la sivyo akatoe ushahidi huo panapohusika! Aache kutulisha longolongo!
Quote
 
 
0 #5 2012-02-01 18:21
Quoting dazu:
Serikali imeshasema kupitia waziri wake wa Uhusiano wa Africa Mashariki kwamba amelishwa sumu. Maana Sitta naye ni serikali, na amewahi kukaimu hata uwaziri mkuu mara kadhaa, Pinda anaposafiri.

da uko sahihi kabsa hiloni tamko la serikali hatuhitaji jingine
Quote
 
 
+1 #4 2012-02-01 17:23
Do!! Tamaa za Ufisadi na wizi wa mali ya Taifa itatufikisha mbait TZ. Wenzetu wako tayali kuuwa, na sio Maalbino tu. Labda bdio maana viongozi wanaogopa kuwashugulikia mafisadi ndani ya Chama na serikali.
Quote
 
 
0 #3 2012-02-01 15:44
Jamani wewe unampa sumu mwenzako kesho wewe ufi?, raiti ungejua utakiachia rahana ya aina gani kizazi chao maana inawezekana wewe ata usiionje hiyo joto ya jiwe, leo unaselebuka lakini kesho yako utajuta tena kuliko yule uliyempa sumu na si ajabu utakuwa umesahau kabisa ulimfanyia nini mwenzio kama rahana hii haitakuandama wewe watoto wako au wajukuu wataandamwa na hii damu inayolia juu yako itabaki adidhi usimuone yule alikuwa ni mtu mkubwa aliwai kuwa mbuge au baba yake alikuwa mtu mzito lakini leo amekwisha, msifanye mchezo hivi vitu vitawaandama mpaka! na hizo damu mlizo zitazitalia juu yenu, watu wanapata ajari kila kukicha wegine ni visasi visasi mtu mmoja anasababisha ajari ya nguvu ukumbuki uliyo mfanyia mwenzio, hivyo hivyo mpaka kizazi kinateketea utatembea kwa wagaga wa kienyeji maana ulizoea mpaka unaona labda MUNGU aliwaumba kwa ajili ya shida kumbe ni wewe unasababisha.
Quote
 
 
+1 #2 2012-02-01 15:31
Quoting dazu:
Serikali imeshasema kupitia waziri wake wa Uhusiano wa Africa Mashariki kwamba amelishwa sumu. Maana Sitta naye ni serikali, na amewahi kukaimu hata uwaziri mkuu mara kadhaa, Pinda anaposafiri.

Nonsense Sitta hakusema kama serikali na ndiyo maana kaambiwa apeleke ushahidi na isitoshe si waziri muhusika wahusika ni waziri wa afya na waziri wa mambo ya ndani ya nchi period! Kama ni kweli Sitta alisema kwa niaba ya serikali basi angeeleza hatua zinazofuata ! Use your brain if you have got one!
Mzalendo!
Quote
 
 
+11 #1 2012-02-01 10:06
Serikali imeshasema kupitia waziri wake wa Uhusiano wa Africa Mashariki kwamba amelishwa sumu. Maana Sitta naye ni serikali, na amewahi kukaimu hata uwaziri mkuu mara kadhaa, Pinda anaposafiri.
Quote
 

Add comment

Tumia jukwaa ili kutoa maoni ambayo yatasaidia kulijenga taifa letu. Kumbuka, maoni yako yatapitiwa kwanza kabla hayajarushwa hewani!!!!!!


Banner
Banner