MwanzoContactsEmail
Home Uchambuzi Uchambuzi na Maoni Juhudi za makusudi zifanyike ili kuepusha migomo hii
BOOKMARK THIS PAGE
Juhudi za makusudi zifanyike ili kuepusha migomo hii  Send to a friend
Thursday, 05 January 2012 20:55

KAMA ni kuuanza vibaya mwaka huu 2012, basi huenda Tanzania itakuwa imejiandika katika historia mbaya kwa matukio haya makubwa mawili ambayo yameanza kujitokeza.

Kwanza , Chama cha Walimu Tanzania (CWT) kimetangaza mgomo wa nchi nzima Jumatatu ijayo kwa wanachama wake kote nchini ambao wanaidai Serikali mabilioni ya fedha zinatokana na stahiki zao mbalimbali.

Jambo la kushangaza, tatizo hilo la malipo ya walimu limechukua sura mbalimbali, kwani huko nyuma, wakati  wa utawala wa Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa liliwahi kuundiwa kamati teule ya Bunge ambayo iliongozwa na aliyekuwa Mbunge wa Babati,  Omari Kwaang’ akisaidwa na Jenista Mhagama (Peramiho).

Ni wazi kuwa baada ya tume ile, Serikali iliahidi kuwalipa walimu baada ya kuhakiki madai yao mbalimbali, ingawa kulikuwa na kauli za kusikitisha na kukatisha tamaa ambazo ziliwahi kutolewa na viongozi wa serikali, wakiwaita walimu kuwa ni wezi, watu wasio waaminifu.

Matamshi hayo ya viongozi wa Serikali yaliwaudhi walimu huku madai yao mbalimbali yakiwa yamewasilishwa ofisi ya Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali (CAG) ambako mengi yalionyesha kuwa halali na kutakiwa walimu hao walipwe.

Kwa nini hawakulipwa hadi sasa? Ni swali ambalo hadi sasa halijapata majibu.
Lakini, kabla ya vumbi la madai ya walimu kutua, sasa limezuka jingine la madaktari na watumishi wengine wa sekta ya afya ambao wametishia kuigomea Serikali ifikapo leo.

Kwa upande wetu, kama wadau na wananchi wa kawaida, tunaamini kuwa mgomo ni silaha ya mwisho ambayo mtumishi anaweza kuitumia kudai haki yake.

Kwa bahati mbaya, hadi sasa baada ya madaktari 229 walioko katika mafunzo ya vitendo kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kuibuka na madai yao, si Serikali wala Wizara ya Afya ambayo imesema lolote kuhusu madai yao.
Tunasikitika kuona hali hiyo ikiendelea katika nchi yetu ambayo tunatambua ugumu wa huduma za afya na jinsi ambavyo wagonjwa wamekuwa wakipoteza maisha kutokana na ukosefu wa huduma hiyo.

Tunapenda kuishauri Wizara ya Afya na Ustawi, chini ya Dakta Haji Mponda ambaye kwa bahati nzuri ni mtaalam wa sekta hiyo na msaidizi wake, Dk Lucy Nkya kwamba wasiogope kukutana na madaktari hao na wawakilishi wao kuepusha mgomo huo ambao utakuwa na madhara makubwa sana kwetu.

Tunaamini kuwa madai ya vijana hao ya posho ya kujikimu ni ya msingi, kwani mbona posho kama zile za wabunge zimekuwa zikipatikana na kulipwa tena kwa wakati, kwa nini si hizi za vijana ambao wako katika mafunzo kwa vitendo.

Tunashauri Serikali kwa umoja wake, ikae chini na kuangalia matumizi ambayo si ya msingi yazuiwe ili fedha zilizopo zitumike kuwalipa vijana hao na kuepusha mgomo huo ambao unaweza kusababisha vifo na madhara mengine kwa mamilioni ya Watanzania.

Migomo hii inatoa picha kwamba serikali yetu imekuwa kiziwi kushughulikia matatizo na kero za wananchi wake kwa muda mrefu na matokeo yake ndiyo matatizo haya ya migomo yanajitokeza.
Kwa mfano haiingii akilini kwamba matatizo ya walimu yamechukua karibu muoingo mmoja bila ya kumalizwa wakati madai yao yanajulikana. Kwa nini?

Kwa upande wa madaktari, hao ni wanataaluma ambao kwa kukatishwa tamaa , wengi wao wanakimbia nchi kwenda ughaibuni, jambo ambalo linawafanya Watanzania kukosa huduma  licha ya nchi kutumia mamilioni ya fedha kuwasomesha.Wakati mwingine baadhi ya wanataaluma hao wameingia katika fani nyingine zikiwamo siasa, biashara kwa sababu ya matatizo yanayosababishwa na serikali yenyewe, ikiwamo ya kutowajali.

Tunadhani sasa ni muda mwafaka kwa serikali kuipatia ufumbuzi haraka kadhia hii ya madaktari na walimu ili kuepusha migomo ambayo haina tija.


Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
Reddit! Del.icio.us! Mixx! Free and Open Source Software News Google! Live! Facebook! StumbleUpon! TwitThis Joomla Free PHP
 

Comments 

 
0 #1 2012-01-06 11:53
Tatzo la nchi yetu n kuzidi kwa ubabaishaji,por ojo na ahadi hewa zszo na tja,utasikia mara ooh tunafanya mchakato,tunaha kik,mara upembuz yakinifu,pesa zipo,cheque znaandaliwa,yaa n maneno tupu vtendo zero,migomo itaisha pind tu viongoz wa serkal yetu watakapoacha kuweka siasa ktk masuala muhimu ya kitaifa,la sivyo migomo hai[NENO BAYA]ma daima.
Quote
 

Add comment

Tumia jukwaa ili kutoa maoni ambayo yatasaidia kulijenga taifa letu. Kumbuka, maoni yako yatapitiwa kwanza kabla hayajarushwa hewani!!!!!!


Banner
Banner