MwanzoContactsEmail
Home Uchambuzi Barua kwa Mhariri Profesa Kahigi kitetee Kiswahili Bungeni
BOOKMARK THIS PAGE
Profesa Kahigi kitetee Kiswahili Bungeni  Send to a friend
Tuesday, 10 January 2012 08:57

Mhariri
NILIFURAHI sana niliposikia mwalimu wangu wa lugha ya Kiswahili na msomi mahiri wa lugha hiyo, Profesa Kulikoyela Kahigi amechaguliwa kuwa Mbunge katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010.
Kwangi nilifurahi kwa kuwa niliamini sasa Bunge letu limempata mmoja wa watu watakaokuwa mstari wa mbele kupigania matumizi ya lugha ya Kiswahili bungeni.

Kwa kweli hali ya sasa katika chombo hicho cha kutunga sheria inatisha, kwani asilimia kubwa ya mazungumzo kwa watunga sheria wetu yamekuwa yakichanganya na lugha ya Kiingereza.
Sijui kama wawakilishi hawa wananchi wanajua kuwa, idadi kubwa ya wafuatiliaji wa mijadala ya Bunge ni wananchi amabo hawan ufahamu wa lugha ya Kiingereza. Inashangaza wao kuendelea kuzungumza huku wakitumia lugha ya kigeni.

Naomba Profesa Kahigi ajue kuwa licha ya kuwawakilisha watu wa jimbo lake na hata kulinda maslahi ya chama chake, bado ana dhima kubwa ya kuitetea lugha ya Kiswahili ambayo kwanza ndiyo iliyompa chati ya kuwa msomi gwiji hapa nchini.
Kama ilivyo kwa wabunge wengine wanaosifika kwa kuwa watetezi wa ufisadi au hata posho za wabunge, namuomba Profesa Kahigi ajipambanue na aanze kuwa mtetezi wa kweli wa Kiswahili.

Awe mstari wa mbele kukemea matumizi ya Kiingereza Bungeni ili wananchi wa kawaida waweze kujua yala yanayojadiliwa na wawakilishi wao.
Njia za kumwezesha kufanya hilo ziko nyingi ikiwamo kuwasilisha hoja binafsi.Kwa kweli inatia aibu kuona Kiingereza kikitamalaki katika mazungumzo ambayo wahusika wake wote wanajua Kiswahili na hata wanaowasikiliza wanaijua lugha hiyo.

Hebu wabunge wetu acheni kasumba na utumwa wa kutumia Kiingereza, na kama kweli mnadhani Kiingereza ndiyo lugha bora, basi amueni kutumia lugha hiyo siku zote na katika vikao vyote.
Naamini hamuwezi kufanya hivyo kwani wengi wenu hamna ufahamu wa kutosha na lugha hiyo. Sasa iweje mng’ang’anie lugha ambayo kumbe hamuijui fika? Profesa Kahigi, tumia hoja hizi kuwaeleza wakubwa wenzako huko Dodoma.
Sanura Bakar
Morogoro


Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
Reddit! Del.icio.us! Mixx! Free and Open Source Software News Google! Live! Facebook! StumbleUpon! TwitThis Joomla Free PHP
 

Comments 

 
0 #1 2012-01-10 15:42
BAKITA wanapaswa kuandaa semina kwa wabunge wote angalau mara moja kwa kila mwaka na kuwashirikisha viongozi waandamizi Bungeni akiwemo Mh. Spika na kiongozi wa shughuli za serikali Bungeni ambaye ni Mh waziri Mkuu kuhusu matumizi ya Kiswahili katika vikao vya bunge. Lakini pia Katiba ya Nchi iliweke wazi swala hili la Matumizi ya lugha ya kiswahili bungeni."TUNAPOIKATAA LUGHA YETU TUSIKATE TUKIITWA WATUMWA."
Quote
 

Add comment

Tumia jukwaa ili kutoa maoni ambayo yatasaidia kulijenga taifa letu. Kumbuka, maoni yako yatapitiwa kwanza kabla hayajarushwa hewani!!!!!!


Banner
Banner