
| ARVS zinazotumika Tanzania zipatiwe mbadala | Send to a friend |
| Friday, 13 January 2012 10:12 |
|
Mhariri NASHUKURU kwa kupata nafasi katika gazeti lako nilipendalo ili niweze kusema machache niliyo nayo kuhusu ugonjwa hatari wa Ukimwi katika Tanzania na dawa za kurefusha maisha, ARVs. Nafahamu kuwa ugonjwa huu haujaingia Tanzania pekee, bali ni Afrika na duniani kote. Lakini wanasema hapa nchini kwetu, ugonjwa huu umefanya mashambulizi na bado unaendelea na mashambulizi hayo. Pamoja na kupatikana kwa dawa hizo za kupunguza makali ya ugonjwa huu, ARVs, lakini bado changamoto zimekuwa nyingi. Kwa mfano, Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) lilitangaza kuwa, dawa hizo hazina usalama kwa asilimia 100. Sasa kama siyo salama kwa kiasi hiki mbona Serikali yetu, hasa Wizara ya Afya ipo kimya wakati Watanzania wengi wanazitumia? Tunaiomba Serikali itafute suluhisho, na si suluhisho la ARVs pekee, bali na tiba kamili ya kutibu ugonjwa huu. Tunataka tiba na si kupunguza makali kwani mpaka hivi sasa watu wameshapoteza fedha nyingi kwenda Loliondo kwa Mchungaji Ambilike Mwasapila na tiba kadha wa kadha lakini hawajapata suluhisho. Si hivyo tu, hizi kampeni za matumizi ya mipira ya kiume nazo zinazidi kuongeza tabia hatarishi kwani ‘condoms’ nazo si kinga ya kuaminika sana. Serikali itusaidie kutafuta tiba ya kuangamiza ugonjwa huu, kwani bila kufanya hivyo taifa lote litamalizika. Fatuma Namwadilanga, |














