
| Walimu watanyanyasika mpaka lini? | Send to a friend |
| Tuesday, 17 January 2012 09:07 |
|
Hii ndiyo Serikali ambayo viongozi wake wengi wanajilimbikizia mali. Wao na familia zao wanaishi kama wako peponi hali wananchi wa kawaida kama walimu tukiteseka kwa kiasi kikubwa. Viongozi wetu kuanzia ngazi za chini hawaelewi matatizo yetu! Kama haitoshi, Serikali inatoa nyaraka za kuwadidimiza, kuwanyanyapaa kuwaondolea utu wao na kuwadharau walimu tena wazi wazi. Mfano ni hivi sasa hata mwalimu akisoma, ngazi yake ya mshahara inabaki palepale! Ewe Waziri wa Utumishi wa Umma na Katibu Mkuu wako. Enyi mawaziri husika na makatibu wakuu, mngekuwa walimu sijui kama mngefurahia mambo haya. Najua aliyeshiba hamjui mwenye njaa, lakini msifanye waziwazi kuionyesha jamii kwamba kazi ya ualimu ni ya kukimbilia tu kama maisha yameshindikana. Naomba muithamini kama kazi nyingine. Maofisa elimu hawazioni nyaraka hizi kama zinawanyanyasa walimu, kwa kuwa wao na familia zao wana maisha mazuri. Wanabaki kusema walimu fanyeni kazi, lakini hawaangalii upande wa pili kwamba walimu wanaishi katika dimbwi la umaskini, hawajui kesho yao itakuwaje. Maofisa hawa wanaangalia matumbo yao na familia zao tu. Namkumbuka Ofisa Elimu mkoa wa katika mkoa mmoja uliopo nyanda za juu kusini, anapoongea na walimu huwa anawachukulia kama watoto wadogo au watoto zake na kuwadharau, kuwadhalilisha hata wale wenye umri kama wa baba yake. Kweli haipendezi na sio sahihi hata kidogo. Nawaomba wasimame kuwatetea walimu na sio kuwakandamiza na kuwadidimiza kila kukicha. Mwalimu Baraka Mushi Mbeya |















Comments
-walim hawajosomea mambo ya mwenge{uhuru torch} lakin ndio wa kwanza kupokea na kupika chakula cha kwenye mwenge
-wao ndio vinara wa kuacha kufanya kazi walizosomea (kufundisha) na kupokea wabunge, mawaziri na viongozi wengine wa kitaifa
-walimu hawana sauti moja [kuna matabaka miongoni mwa wale wenye vyeti, stashahada na wale wenyeshahada.
wangekuwa na sauti moja wangefanya maamuzi magum walipoitwa makanjanja na mbayuwayu.
lazima wanyanyasike.