
| Leseni mpya ni kukusanya mapato, kulinda ajira za madereva au kupunguza ajali? | Send to a friend |
| Thursday, 19 January 2012 10:37 |
|
Na Zakie Chatanda Sababu kubwa ya ajali ilitajwa kuwa leseni nyingi hasa zile za daraja la C ama zilitolewa kwa wasiostahili au wengi walizipata kwa njia za ujanja ujanja. Hatua hiyo ingesaidia kubaini leseni bandia na zilizotolewa bila ya wahusika kufanyiwa bila kupitia mafunzo maalum na kuruhusu kuanzishwa kwa mfumo wa kisasa wa kutunza kumbukumbu za leseni na madereva vizuri. Suala la pili ilikuwa ni kuboresha leseni yaani kuondokana na mfumo wa sasa ambao ni wa kizamani na kuzibadilisha kuwa katika mtindo wa kisasa yaani za kielektronika. Mfumo utakuwa rahisi kujua taarifa za kila ambaye ana leseni ya kuendesha gari nchini. Suala la tatu ni kusaidia kutunza kumbukumbu za madereva na leseni zao baada ya kubadilisha leseni kwani asilimia kubwa leseni zilizotolewa zamani takwimu zake zilikuwa zinahifadhiwa kwenye vitabu hivyo ilikuwa ni vigumu hata kujua idadi ya madereva nchini. Hatuna budi kuipongeza serikali, Mamlaka ya Mapato (TRA) pamoja na Jeshi la Polisi kwa hatua hii nzuri kwani mbali na kupunguza au kutokomeza ajali nchini pia leseni za madereva wetu zitakuwa zina mvuto, muundo wa kisasa na vile vile kumbukumbu zao zitakuzwa zinahifadhiwa kisasa zaidi. Dosari la hii kazi kubwa inakuja pale tu, serikali inapotaka kugeuza shughuli hii kwa ajili ya kukusanya mapato zaidi na hivyo kufifisha madhumuni yake tuliyoambiwa wakati wa kutangazwa kwa nia ya kuanzisha zoezi hilo. Ada kwa ajili ya mafunzo hayo ambayo yanachukua siku 10 tu inafikia Sh200,000. Kiwango hicho ni kikubwa mno na gharama zake haziwiani na mafunzo mafunzo anayohitaji dereva mzoefu wala hata na vipato vya madereva wengi nchini. Serikali inapaswa kukumbuka mara kadhaa madereva hao wametishia kugoma kutokana na ujira mdogo kutoka kwa wajiri wao. Ninaamini kuwa madereva wengi watakosa fursa ya kubadilisha leseni kwa kutokuwa na fedha. Hii itawafanya wengi kusaka vyeti kwa njia ya mkato ili waweze kubadilisha leseni zao au wengine watabaki majumbani na hivyo kuongeza jeshi la wasio na kazi nchini. Jambo jingine ambalo ninaliona kuwa ni dosari kubwa katika zoezi zima la kubadilisha leseni ni kitendo cha kuwataka kufanya hivyo hata kama kama zile walizonazo hazijamalizika muda wake. Ni leseni zilizotolewa na mamlaka hiyo hiyo. Hii maana yake ni nini? Ningeelewa kama zoezi hilo lingewagusa wale ambao leseni zao zimekwisha muda. Katika hili serikali imekosea ilipaswa kuheshimu ukomo wa leseni ilizozitoa ili dereva akitaka kuongeza muda ‘renew’ ndiyo apewe leseni mpya badala ya ile ya zamani hii itaondoa machungu kwa baadhi ya madereva kwa sababu wengi wao leseni zao wamebadilisha mwaka jana na inatakiwa wakae nazo miaka mitatu kabla ya miaka hiyo haijaisha au hata miezi sita wanaambiwa kuzibadilisha tena kwa gharama kubwa zaidi na baada ya mafunzo maalum. Madereva wengi wameshindwa kubadilisha leseni zao katika muda uliopangwa wa Desemba 31, 2011. Jambo hilo lisababisha tafrani na taharuki pale mabasi mengi yaliposhindwa kufanya safari kwa kuwa madereva wengi hawakuwa na leseni mpya. Januari 6, 2012 serikali ililazmika kuongeza muda bila kutaja ukomo wake. Kuliko hivi sasa serikali kuwakimbiza kimbiza madereva kubadilisha leseni kitu ambacho mimi binafsi naona ni kibaya kwani kinaongeza mianya ya rushwa sehemu za kubadilishia leseni pamoja na vyuoni kwani madereva wengi watanunua vyeti badala ya kupata elimu husika. Hili la kuwataka madereva kubadilishe leseni zao huku serikali ikijua kuwa bado hazijaisha muda siyo utawala bora na wengi tunaitafsiri hatua hii kuwa ni mkakati wa serikali wa kukusanya pesa kutoka kwa watanzania ambao tayari wanakabiliwa na maisha magumu. Tunadhani serikali inapaswa kutafuta njia nyingienya kutafuta pesa kwa ajili ya kuendesha nchi pasi na kuwatia jakamoyo wananchi. Zoezi hili la kubadilisha leseni ni kero. Ni zoezi ambalo halitapunguza ajali wala kuboresha ajira za madereva nchini Tanzania. |















Comments
Tunao majirani zetu kama Kongo,Luanda,Ke nya,Uganda. Wanafuata Kanuni na Sheria vema sana, tofauti na Tanzania/Tanganyika. Hapa ni mchanganyiko wa vitisho na Uroho wa Rushwa tupu kuharibu hata baadhi ya makusudio mazuri yanaingia pabaya kila siku.pia tunaishi kwa MAtukio/Ajari hapo kila kiongozi hujaribu kutoa matamko makali.Jeshi la polisi livunjwe na kuundwa upya kama taasisi.
Tulikuwa na system ambayo ingeongeza tija katika tatizo la ajali RATIBA ZA MUDA WA SAFARI lakini wapi bwana nani anajuazilipo fia,hapa ni kutafuta hela na si vinginevyo,hivi tujaribu kuulizana nani atakae kuwa anajua dereva fulani kafungiwa kuendesha magari kutokana na ajali,hivi dereva huyu akitoka dar-moshi akaenda masasi-mtwara kuna raia atakae mtambua?jibu hapana ni traffic police pekee nae tena mpaka amkamate na kosa waende kituoni ndio atakuwa na jinsi ya kumtambua,na kwa dereva kwenda kituoni wakati unajua leseni yako imeshafungiwa haitawezekana mtayamaliza na askari pembeni sasa pana nini hapo.Kama msoni alie elimika anataka maisha ya anasa ndani ya miaka yake michache ya ajira ndivyo kwa hata askari wetu je ninani atakae simamia sheria