
| Bwagamoyo:Igunda kipimo sahihi cha siasa za CCM, Chadema | Send to a friend |
| Saturday, 10 September 2011 17:07 |
|
L. W. Nzela MATOKEO ya uchaguzi mdogo katika Jimbo Igunga yatatoa jibu sahihi ya ni siasa za chama gani zinakubalika zaidi nchini sasa hivi. Uchaguzi huu mdogo ambao kampenzi zake zimeanza wiki hii unafanyika kufuatia kujiuzulu kwa mbunge wa muda mrefu wa jimbo hilo kwa tiketi ya CCM, Rostam Aziz kufuatia shinikizo kubwa la kuhusishwa kwake na kashfa mbalimbali za kifisadi nchini na mgongano wa kisiasa ndani ya chama hicho. Baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana vyama vikuu vya siasa nchini CCM na Chadem viliamua kufanya siasa tofauti ambazo zimeendelea kuligawa taifa. Siasa hizi zinaenda kujaribiwa matokeo yake huko Igunda kwani siasa zenyewe zimetokana na kukuzwa kwa namna moja au nyingine na Rostam Aziz akiwa mbunge na yumkini mwanasiasa mwenye nguvu zaidi ndani ya CCN. Kwa wa CCM siasa zake zilijikuta zikipoteza mvuto kuliko wakati mwingine wowote wa historia yake. Siasa zake zilijengwa katika msingi wa kile tunachoweza kukiita “kuonesha mafanikio” ya CCM, hivyo walitumia muda mrefu kuelezea na kuwafanya watu waone “mafanikio” na kuwa kwa kufanya hivyo basi wapiga kura wataona sababu ya kuendelea kuichagua CCM. Ni katika mwelekeo wa mawazo hayo viongozi wa CCM walijikita katika kubeza wale ambao “hawaoni mazuri yaliyofanywa na CCM” na hivyo kuwafanya watu waone mazuri na wakiona mazuri wakubali kuwachagua wagombea wake. Naamini ni mkakati huu huu utatumika tena Igunga. CCM itajaribu kuonyesha mambo mbalimbali ambayo yamefanywa na Serikali hiyo, mbunge aliyejiuzulu na hata Serikali ziliopita huko Igunga. CCM itajihidi kuonyesha kuwa siasa za mahali (local politics) za pale Igunga zinaonesha pasipo shaka kuwa CCM inakubalika kwani imefanya mengi. Ili hoja hii ifanikiwe hata hivyo naamini itabidi iwe tofauti na hoja zilizopita ambapo wingi wa vitu vilivyofanywa na CCM ndio ulikuwa unatiliwa mkazo zaidi. Kwamba Serikali imejenga shule nyingi, kliniki nyingi, wanafunzi wengi, barabara nyingi, n.k Tatizo la hoja za wingi ni kuwa watu wataanza kuuliza ubora. Je, katika hivyo vitu vingi ni vipi viko bora? Je, elimu inayotolewa ni bora kiasi gani? Je, wanafunzi kwenye hizo shule nyingi wanafauli kwa kiasi gani kulinganishwa na wanafunzi wa sehemu nyingine? Haya ni maswali ambayo upinzani unaweza kabisa kuyatumia kubomoa hoja ya “mafanikio”. Lakini CCM haikuishia hapo. Baada ya kufanya vibaya kwenye uchaguzi uliopita kulinganisha na chaguzi zilizotangulia CCM iliamua kuanza kujichunguza na kujisafisha katika kile ambacho kinajulikana kwa umaarufu kama “kujivua gamba”. Jinsi jambo hilo lilivyopigiwa panda wakati wake kulifanya watu waamini kabisa kuwa ni wakati wa CCM kujisafisha na hasa pale ambapo mafisadi ndani ya chama hicho iliposemwa kuwa wamepewa siku tisini kujiuzulu nafasi zao. Kwa kadiri siku zilivyozidi kwenda ndivyo maana ya kujivua gamba ilipozidi kupanuliwa na kufafanuliwa zaidi na zile siku tisini zilipopita ikajulikana wazi kuwa juhudi za kujivua gamba hazikuwa rahisi tena. Hili la CCM kushindwa kujisafisha hadi kupata hisani ya Rostam kujiuzulu mwenyewe huko wenzake wakiweka ngumu kunaweza kutumiwa vizuri kabisa na upinzani kuonesha jinsi gani CCM imekuwa dhaifu na kwamba siyo ile CCM ambayo wanaigunga walikuwa wanaifahamu zamani. Kwa upande wa Chadema siasa zake kabla ya uchaguzi mkuu zilikuwa katika kuonesha udhaifu na ubovu wa nchi chini ya CCM. Kwa kifupi Chadema ilijaribu kuonyesha kuwa kile kinachoitwa “mafanikio” kilikuwa ni “majaribio yaliyoshindwa”. Kwa muda mrefu walifanikiwa sana kuonesha kuwa kama CCM ingeweza kutawala vizuri zaidi na kusimamia vizuri raslimali zetu Tanzania ingekuwa zaidi ya ilipo sasa. Kimsingi, CDM walikataa kukubali kuwa tulipo hapa kama taifa ni matokeo ya kazi nzuri ya uongozi wa CCM. Hoja hii ilikubaliwa sana, kwani wakitumia mifano ya nyumba za tembe na matatizo ya wananchi waliweza kuwashawishi wananchi kuwa walichokipata sicho walichokistahili. Kwamba tatizo halikuwa kukosekana tu kwa shule za kata bali ubora wa shule hizo, kwamba tatizo halikuwa kukosekana tu kwa vitu bali ubora wa vitu vilivyopo. Na walienda mbele zaidi kwamba, baadhi ya matatizo yalisababishwa na vigogo wa CCM na ni matatizo ambayo yalikuwa na matokeo ya moja kwa moja katika maisha ya Watanzania. Hivyo, walipotangaza orodha yao ya aibu ya mafisadi na walipowakomalia kina Chenge, Rostam, Mkapa, Lowassa na wengine ilikuwa ni katika kuonyesha kuwa matatizo ya Watanzania yanahusiana moja kwa moja na baadhi ya vigogo wa chama tawala. Matokeo yake Chadema ikajikuta inajizolea kura nyingi zaidi na kukubalika zaidi kuanzia vijijini na mijini. Na baada ya uchaguzi huo ChademaM ikaamua kuchukua siasa za migongano (confrontational politics) kuanzia kususia hotuba ya Rais Kikwete Bungeni Dodoma kwenye kikao cha kwanza cha Bunge hili na baadaye kampeni za maandamano za kufanya mashinikizo mbalimbali na kufanya watawala wakose raha kabisa. Siasa hizi za migongano na maandamano zitaenda kujaribiwa matokeo yake huko Igunga. Lakini siasa hizi zinaweza kutumiwa vizuri tu kinyume na CCM kwa kuonyesha kuwa siasa za migongano zina matokeo mabaya kwa jamii wakitolea mifano ya Syria na Libya na wakati huo huo kuonyesha kuwa Chadema inachochea “nchi isitawalike”. Kama CCM ikijipanga vizuri kuonesha madhaifu ya Chadema kama chama na kuwa kinakabiliwa na changamoto zile zile za zamani kinaweza kupunguza makali yake. Kwa mfano, suala la posho za vikao linaweza kutumiwa vizuri kabisa na CCM kuonesha kuwa Chadema kama chama hakina msimamo mmoja wala hakiwezi kusimama pamoja. Mgongano wa nani anapokea posho na nani anataka posho japo unaweza kutajwa ni ‘tofauti za kisiasa’ umeonesha tu kuwa kuwa siyo wote ndani ya Chadema wanaaamini kile ambacho chama kinaamini kwenye mambo ya msingi. Mgongano wao na Shibuda ni mgongano ambao unaweza kutumiwa vizuri na CCM. Kwa ufupi ni kuwa atakayeshinda Igunga atakuwa siyo yule aliyeimba sana au aliyekuwa na watu wengi kwenye mikutano yake bali yule aliyeweza kumfanya mwenzake akataliwe na asikubalike. Yaani, yule ambaye kwa upande wa CCM ataweza kuzileta siasa za mahali na kuzipa matumaini ya siasa za kitaifa na kwa upande wa Chadema siasa za kitaifa na kuzileta kuzipa mwanga wa siasa za mahali. Nani atashinda? Naamini baada ya kama wiki mbili za kampeni tutapata picha nzuri ya nani anaelekea kuvutia watu zaidi kwa hoja zake. Tutaweza kutabiri kwa uhakika zaidi wakati huo. Niandikie:
This e-mail address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it
|















Comments
Madhaifu ni madhaifu tu hakuna dhambi ndogo. Kumbuka wafadhili wa cdm ni makapi ya ccm. (Mrema Arusha, Maswa, Na wahindi wanaowapa mamilioni ili mkiingia mmwape makandarasi. nani asiyewafahamu?)
youtube.com/.../...">