|
Hatuwezi kukuza soka la Tanzania kwa kuzifadhili Simba na Yanga |
Send to a friend |
|
Monday, 26 September 2011 09:29 |
|
Aidan Mhando MCHEZO wa mpira wa miguu ni miongoni mwa michezo inayopendwa na watu wengi hapa nchi na kupelekea kuwa na mashabiki wengi wanaongezeka kila kukicha.
Lakini naamini ya kwamba mpira wa miguu au soka ni miongoni mwa ajira nzuri kwa vijana hasa kipindi hiki ambacho makampuni mengi ulimwenguni yanajitokeza kufadhili mchezo huu na kuzidi kuwashawishi vijana kujikita katika fani hiyo.
Hata kumekuwa na matatizo ya timu nyingi ambazo zinashiriki katika ligi guu ya Tanzania bara inayojulikana kama ligi ya Vodacom, kulalamikia kukosa wafadhili hali inayosababisha klabu hizo kutofanya vizuri kwa sababu ya kushindwa kujiendesha kwa kukosa fedha.
Huu ni ukweli usiopingika kwamba mchezo wowote duniani lazima uwe na wafadhili ndipo utakapo kuwa na mafanikio sasa imefika wakati kwa wadau wasoka nchini kuiga mifano kutoka katika nchi ambazo zimepiga hatua katika mchezo soka kwa kujitokeza kufadhili timu ndogo ambazo hazina wafadhili.
Baadhi ya timu hapa nchini ambazo hazina wafadhili zimekuwa zikifanya vibaya kwa sababu ya kushindwa kujiendesha hii yote ni kwa sababu ya kukosa mahitaji muhimu ya kuiendesha timu.
Kwa sababu timu hizi zimekuwa zikitegemea viingilio vya uwanjani ndipo zipate fedha za kujiendesha hali nayowawia vigumu kufanya vizuri katika ligi.
Kumekuwa na matatizo kwa wachezaji kutolipwa mishahara yao kwa wakati hii yote ni kwa sababu ya kukosekana kwa wafadhili lakini mataizo kama haya tunaweza kuyapunguza au kuyaondoa kabisa kama wadau wasoka watajitokeza kuzisaidia timu ndogo.
Lakini pia matatizo haya yote yanatokana na sisi wenyewe kuwa na mapenzi ya timu za Simba na Yanga hali inayopelekea kusahaulika kwa timu nyingine ambazo nazo zinaitaji wafadhili.
Kama tunataka soka la Tanzania likuwe kimataifa basi sasa imefika wakati kwa wadau wasoka kujitokeza kufadhili timu ndogo ambazo nazo zinashiriki katika ligi kuu kama tutaweza kufanya hivyo tuweza kuliinua soka la Tanzania kwa kiwango cha kikubwa.
Hata hivyo kwa upande mwingine sababu ambayo inapelekea wachezaji wengi wa Tanzania kushindwa kufikia viwango vya kimataifa ni kwa sababu ya kuangalia upande mmoja yani ili mchezaji aweze kupelekwa kufanya majaribio nje ya nchi ni lazima achezee klabu kubwa zikiwemo Yanga na Simba.
Kama tutawawezesha wachezaji wanaochezea katika timu ndogo kwa kuwapatia vifaa mbalimbali vya michezo ikiwemo na kuwatengenezea mazingira mazuri ya kupata mahitaji muhimu tunaweza kutengeneza kizazi cha soka ambacho kinaweza kuiletea sifa kubwa taifa.
Leo tunashuhudia katika ligi mbalimbali za wenzetu Afrika timu ndogo zinakuwa na wafadhili wakubwa ambao wanaziwezesha timu hizo kushiriki vizuri katika ligi na hatimaye kuwapelekea kufanya vizuri kimataifa.
Soka la Tanzania kamwe haliwezi kufanya vizuri kama tutaegemea upande mmoja wa kuziwezesha timu kubwa na kuziacha timu ndogo zikiwa hazina uwezo wa kujiendesha.
Imefika wakati sasa kwa klabu za samba na Yanga ambazo ni klabu kongwe kuzipa nafasi timu ndogo ili nazo ziweze kupata ufadhili na hatimaye kutengeneza vijana wenye uwezo mkubwa katika soka.
Pia Shirikisho la soka nchini (TFF) nalo linanafasi ya kuwahamasisha wadau wasoka kujitokeza kuzisaidia timu ndogo ambazo nazo zinashiriki katika ligi kuu hapa nchini naamini kwamba kupitia uhamasishaji wao wafadhili wengi watajitokeza na kuzisaidia timu hizo.
Inasikitisha sana pale timu inapo tumia nguvu nyingi kuhakikisha inapanda daraja na kushiriki ligi kuu lakini baadaye inashuka daraja kwa sababu ya kukosa fedha za kujiendesha hili ni jambo la kusikitisha.
Nadhani sasa wakati umefika kwa TFF, klabu kufanya juhudi za makusudi kuomba kufanyika kwa marekebisho ya Katiba ya nchi kwa mujibu wa Baraza la Michecho Tanzania ambayo inatambua klabu na chama hicho kuwa ni vyama vya hisani 'Amatuech'.
TFF na klabu zetu zinashindwa kufanya mabadiliko makubwa ya kufikia maendeleo kwa sababu ya kubanwa na kipengere hichi kinachoonyesha kuwa michezo ni jambo la hisani.
Kuepuka hili ni lazima TFF na klabu kukubali kujisajili upya kwenye wizara ya kazi na kutambulika kama kampuni ili ziweze kuwavutia wawekezaji wengi.
Nilifikiri TFF walipoamua kuibadilisha ligi kutoka ligi daraja la kwanza na kuwa Ligi Kuu waliangalia jambo hili kama walivyofanya wenzao wa Kenya na sehemu mbalimbalii ambao wameanzisha Kampuni ya kuongoza Ligi Kuu ikiwa nje ya shirikisho.
|
Comments
Suala la kukosa udhamini yaweza kuwa moja ya sababu zinazofanya timu nyingine zihangaike lakini sio sababu pekee. Kwa mfano, ligi ya Hispania ambayo ni moja ya ligi bora duniani ina timu nane zisizo na udhamini wa jezi. Klabu tunazozifahamu kwa ubora wao wa soka kama Valencia (washindi wa tatu wa La Liga 2010-2011), Atletico Madrid (mabingwa wa kombe la Europa na Super Cup 2009-2010), Villareal na Sevilla hazina udhamini wa jezi lakini zimekuwa zikitoa ushindani mzuri ndani na nje ya Hispania.
Tunahitaji mikakati endelevu kuendelea lakini kila tuna shida ya kuangalia leo tu.