Kulikoni kesi ya Mbowe na Matiko

Sunday December 2 2018

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Mbunge

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko (mbele kulia) wakiwa chini ya ulinzi wa askari Magereza walipofikishwa katika Mahakama Kuu ya jijini Dar es Salaam jana, kusikiliza rufaa yao ya kupinga uamuzi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa kuwafutia dhamana, katika kesi ya jinai inayowakabili. Picha na Anthony Siame 

Mhariri,

Mimi sio mwanasheria lakini napata wakati mgumu ninapotafakari juu sheria na wanasheria upande wa serikali juu ya kesi Kiongozi wa Upinzani bungeni, Freeman Mbowe na Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko.

Watu wanaowang’ang’ania kimsingi hawajaiba, hawajaua na wala hawajamdhulu mtu yeyote. Kosa lao kubwa ni kukiuka utaratibu ambalo kimsingi halijasababisha madhara yoyote.

Sioni mantiki ya kinachoendelea. Hebu kuweni makini. Kumbuka hawa mnaowang’ang’ania kuwaweka mahabusu kwa sababu zisizo na msingi wana familia kama ilivyo kwenu!

Sijui tunaelekea wapi na mwisho wa yote haya utakuwaje, lakini hatuwezi kujenga umoja na mshikamano wa kitaifa kwa staili hii.

Tija ya kuwang’ang’ania hawa ni ipi? Kwamba wakikaa ndani kama Taifa tutanufaika na chochote.

Tunahitaji umoja katika maamuzi katika kila nyanja yenye tija kwa Taifa. Tunahitaji kujenga nchi yetu kwa ushirikiano.

Mwalimu Malik,

Dar