Je, Kazi Yako Ipo Hatarini? Kazi 7 Zinazoelekea Kutoweka

Wednesday December 13 2017

Sehemu ya tovuti ya BrigherMonday ambayo

Sehemu ya tovuti ya BrigherMonday ambayo inakuruhusu kuingia na kutafuta kazi uipendayo mcl

Kadri teknolojia inavyokua, sifa muhimu za mwombaji kazi zinazidi kubadilika. Kwa sasa ili uweze kuwa mshindani kwenye soko la ajira ni lazima uwe na ujuzi wa kidigitali. Lazima ujue kutumia kompyuta, intaneti na mitandao ya kijamii. Utafiti uliofanywa na Nesta unaonyesha kuwa asilimia 10 ya walioajiriwa katika fani yeyote wanatarajiwa kukua kikazi, huku asilimia 20 wakitarajiwa kukosa kazi. Ajira katika sekta ya Elimu na Huduma za Afya zinatarajiwa kuongezeka. Hii ni kwa sababu mahitaji ya sekta hizi yanatarajiwa kuongezeka. Kwa baadhi ya sekta mahitaji yanatarajiwa kupungua na hivyo kazi kuwa haba. BrighterMonday imeorodhesha chini baadhi ya kazi zinazotarajiwa kutoweka.

Madereva wa Teksi na Vyombo Vingine vya Usafiri

Teknolojia katika sekta ya uchukuzi inakua kwa kasi. Makampuni kama Waymo tayari yanafanya majaribio ya magari yanayojiendesha bila dereva. Wataalamu wanatabiri kuwa katika miaka ya karibuni tutaanza kuona teksi zisizokuwa na madereva. Kwenye usafirishaji wa bidhaa, ndege ndogo za midoli (drones) zimeshaanza kusafirisha bidhaa kwenda kwa wanunuzi. Zipline, kampuni inayotoa huduma ya dawa za dharura pale zinapohitajika kwa kutumia drones, tayari imeshatangaza kuanzisha huduma zake nchini Tanzania.

Wahasibu

Wataalamu wanatabiri kuwa, paka kufikia mwaka 2028 kazi za uhasibu zitakua zimetoweka. Programu za uhasibu kama Quickbooks na Quill zinakua kwa kasi katika sekta hii. Utegemezi wa wamiliki wa biashara kwa wahasibu unaendelea kupungua. Programu za uhasibu zinawawezesha wamiliki wa biashara kupata taarifa zao mahala popote na kwa urahisi. Programu hizi zinachambua na kuwasilisha taarifa katika namna ambayo mtu ambaye sio mhasibu anaweza kuelewa kwa urahisi. Kadri teknolojia inavyokua programu hizi zinatarajiwa kupata ujuzi kushinda wahasibu.

Wafasiri

Zana zinazotumika kutafsiri zinakua kwa kasi, na zinakuwa rahisi kupatikana. Programu za simu, tovuti na programu za kivinjari zinazotumika kutafsiri zinaongezeka kwa kasi na zinazidi kuwa sahihi kwenye tafsiri zake. Imekuwa ni rahisi zaidi kutumia zana hizi kutafsiri kuliko kuajiri mfasiri. Hii inaonyesha ni jinsi gani kazi za wafasiri zipo hatarini.

Wafanyakazi wa Posta

Mara ya mwisho kupokea barua ni lini? Kadri miaka inavyosogea, barua pepe inazidi kua njia kuu ya kutuma ujumbe. Mwaka 2015 idadi ya barua pepe zinazotumwa na kupokelewa kwa siku ilifika zaidi ya bilioni 205. Ongezeko la kampuni binafsi za usafirishaji wa bidhaa pia kumepelekea kuzorota kwa huduma za posta sababu ya ushindani mkali. Haya yote pamoja na kuanzishwa kwa mashine maalum za kupangilia barua kunaweka wazi kuwa kazi za posta zinaelekea kutoweka.

Wasajili

Kiasi cha data kimekua kikiongezeka hivi karibuni. Haja ya kuajiri mtu kwa ajili ya kuhamisha au kuingiza data imekuwa ikipungua. Vyote hivi vinaweza kufanywa kiurahisi kwa kutumia teknolojia kama skana, vitambuzi sauti na vitambuzi picha. Ili kupunguza gharama kampuni zimepunguza kuajiri na badala yake zinawekeza kwenye teknolojia hizi.

Matangazo ya Simu

Matangazo ya barua pepe na ya mitandao ya kijamii yameongezeka kwa wingi katika miaka ya karibuni. Hii imepelekea kupungua kwa matangazo ya simu. Imekuwa ni ngumu zaidi kwa watu kupokea simu kutoka kwa namba wasizozijua. Hii inapelekea makampuni kutengeneza programu za kufanya kazi hii ili kupunguza gharama. Hii ndio sababu kuu ya kutoweka kwa sekta hii.

Wakala wa Safari

Teknolojia ya intaneti imepelekea kuibuka kwa tovuti kama Airbnb, TravelStart na nyinginezo. Tovuti hizi zinaondoa haja ya kuwepo kwa wakala wa safari. Sasa, unaweza kupanga safari yako bila kutumia huduma za wakala wa safari. Shughuli za kukata tiketi au kutafuta hoteli zinaweza kufanywa mtandaoni bila haja ya wakala wa safari.

Usikate Tamaa

Ingawa kazi zote hazikai milele, uzoefu ulionao utakusaidia pale unapotafuta kazi nyingine. Lakini, ni muhimu uongeze ujuzi wako katika sekta tofauti tofauti ili uweze kushindana katika soko la ajira. Jiunge na BrighterMonday ili upate taarifa mpya kuhusu soko la ajira na nafasi za kazi zilizopo.