Jinsi ya Kuandika Barua ya Maombi ya Kazi Ambayo Mwajiri Hawezi Kuipuuza

Friday December 29 2017

Uandishi wa barua ya maombi ya kazi inawezekana

Uandishi wa barua ya maombi ya kazi inawezekana usione ni jambola maana. Lakini barua iliyoandikwa vizuri itakuza nafasi yako ya kupata kazi. Dondoo hizi zitakusaidia  kuandika vizuri na  ujue umuhimu wa kuandika barua hiyo. MCL

Hivyo hata kama mwajiri wako asipo omba barua, ni jambo zuri kuandika barua kwa hiari. Ni kazi ngumu, lakini uandishi wa barua utafanya maombi yako ya kazi yawe ya kipekee. Mtaalamu wetu wa rasilimali watu, Gizzel Mbaga alichangia ufahamu zaidi kuhusu nini unachohitaji ili uwe na barua ya maombi nzuri.

Barua za Maombi Zinaja Wasifu Wako

Kosa kubwa unaloweza kulifanya kwenye uandishi wa baru ya maombi ni kuiandika kama insha ya CV/Wasifu wako. Ukifanya hivi basi hakika barua yako itatupwa. Hivyo badala ya kukopi CV yako barua yako ya maombi inatakiwa iijazie CV yako kwenye sehemu za muhimu au ambazo zimeandikwa kwa ufupi kwenye CV, hizi ni kama

•    Mapengo katika uzoefu wako wa kazi
•    Shahada za chuo ambazo haziendani na kazi unayofanya
•    Mabadiliko ya ghafla ya taaluma(au kama hujawahi kufanyakazi kwenye aina ya nafasi unayo omba kazi)
•    Uzoefu mwingine uliopata nje ya kazi ambao utakusaidia kwenye kazi uliyoomba( kusafiri, kujitolea, kazi za kujitolea)

    Barua ya Maombi Inaeleza Historia

Barua yako ya maombi inaonyesha taarifa ambazo hazipo kwenye CV yako. Inatoa fursa ya kuelezea kuhusu mabadiliko yako na maendeleo yako katika taaluma yako.
So, while your resume can show that you’ve gotten better job positions over the years
Hivyo, wakati CV yako inaonyesha nafasi za kazi ulizofanya katika miaka iliyopita (nafasi ya chini > mfanyakazi mshirika > msimamizi).  Barua yako ya maombi ndio mahala pa kuelezea jinsi hili lilivyotokea na ujionyeshe vizuri (bila kudanganya).

   Barua za Maombi Zinaonyesha Unaweza Kujieleza Vizuri

Haijalishi ni kazi gani au taaluma gani uliyokuwepo, kama unafanya kazi inayohitaji ujuzi wa kitaalamu. Ni muhimu kuweza kuwasiliana vizuri. Hii itakusaidia unapoandika barua pepe, ripoti za miradi na vinginevyo. Mwajiri atatumia barua yako ya maombi kupima uwezo wako wa kueleza fikra zako na kuzitetea. Baadhi ya miongozo ya kuweza kujielezea vizuri ni,
•    Mpangilio unaoeleweka: mwanzo, sehemu kuu na hitimisho
•    Isiwe na makosa ya kisarifu au tahajia
•    Iwe na taarifa ambazo hazipo kwenye CV

Sasa umeshajua jinsi gani barua ya kuomba kazi inaweza kumsaidia mwajiri wako mtarajiwa akujue zaidi, kwa nini usiandike moja?

Mwongozo wa Hatua kwa Hatua Jinsi ya Kuandika Barua ya Maombi

1.     Anuani

Andika anuani yako upande wa kulia juu kwenye barua yako, anuani iwe na:

•    Jina
•    Mahala Unapoishi
•    Namba ya Simu na Barua Pepe

Weka anuani ya mtu unaemtumia  barua upande wa kulia juu ya barua yako (mkabala na anuani yako). Kazi nyingi hazikupi mtu maalumu wa kumtumia barua, lakini unaweza ukajiribu kutafuta ni nani atakayesoma barua yako kwa:

•    Tembelea tovuti ya kampuni na mtafute afisa rasilimali watu au msimamizi wa nafasi ya kazi unayoomba.
•    Tumia LinkedIn kugundua wafanyakazi wa kampuni unayoomba kazi
•    Wapigie kampuni omba kuongea na afisa wa rasilimali watu na uulize uiandike barua kwenda kwa nani
•    
2.     Andika Kwa Mtu Maalumu

Jitihada ulizofanya kutafuta mtu wa kumwandikia barua zitakusaidia pale unapoandika anuani. Maafisa rasilimali watu kote watakwambia ni vyema kuiandika barua yako kwenda kwa mtu maalumu, mfano,”Kwenda kwa Bi. Serengia..” au “Kwenda kwa Dkt. Evans..” kuliko kuandika “Kwenda kwa mhusika..”

3.     Utangulizi

Your first paragraph should first state what position you are applying for. Aya yako ya kwanza inatakiwa iseme ni kazi gani umeomba. Mara nyingi waajiri wanakuwa wanaajiri nafasi tofauti kwa wakati mmoja, hii pamoja na idadi ya maombi wanayopokea inaweza kuwafanya wasahau ni kazi gani amabyo unaomba. Baada ya kuandika hivyo elezea kwa nini unataka kufanya kazi iliyotangazwa na kwa nini unataka kufanya kazikwenye kampuni hiyo. Hii itakulazimu ufanye uchunguzi kidogo kuhusiana na kampuni hiyo.

4.     Sehemu Kuu

Aya mbili zinazofuata za barua yako ni nafasi ya wewe kujielezea kwa nini ni chaguo zuri kwa kazi hiyo. Kumbuka, sio lazima uongelee kila kazi uliyoweka kwenye CV yako, badala yake, chagua zile ambazo zimekupa ujuzi unaohitajika kwenye kazi unayoomba. Zielezee historia yake vizuri.

5.     Hitimisho

Hitimisho linatakiwa lirudie kwa ufupi kwa nini unataka kufanya kazi iliyotangazwa, na utoe taarifa zako za mawasiliano. Unaweza kuandika kama:

“Nikiwa na uzoefu wa zaidi ya miaka 5 katika mauzo, uwezo wangu wa kuuza mtaani na kusimamia timu umeinandaa vizuri kujiunga na timu ya mauzo ya BrighterMonday kama Meneja Mauzo. Nina hamu kubwa ya kufanya kazi kwenye moja ya biashara za mtandaoni inayoaminika nchini, kama mngependa kufanya kazi na mimi basi tunaweza kuwasiliana kupitia +255784567890.

Wako katika kazi,

Anna Mallo

(amb: CV)”

Umefanya kazi kwa juhudi kwenye barua yako, usiharibu nafasi zako za kumvutia muajiri kwa kutofata utaratibu. Ukipewa barua pepe ya kutuma maombi na ukaambiwa uweke kichwa fulani cha habari, basi fanya hivyo. Ukipewa tarehe ya mwisho ya kutuma, basi hakikisha umetuma kabla haijafika. Kumbuka barua ya maombi sio mbadala kwa nyaraka nyingine za maombi kama sampuli za kazi, vyeti au CV. Pia unapotuma maombi yako kwa barua pepe basi kwenye ujumbe weka sehemu kuu ya barua yako ya maombi ili kuongeza nafasi ya afisa rasilimali watu kuisoma.
Uko tayari kutengeneza barua ya maombi itakayo kupatia kazi unayoitaka 2018? Iandike pamoja na CV yako na uiweke BrighterMonday.