Faida za majani, mizizi ya mlonge

Kila sehemu ya mti wa mlonge hutumika kwa dawa. Majani ya mlonge yanaweza kutafunwa mabichi, yaliyochemshwa kama mboga au yaliyokaushwa na kusagwa kuwa unga.

Mlonge una vitamini A zaidi ya ile ya kwenye karoti na protini nyingi kuliko mtindi.

Pia, una madini chuma, asidi amino muhimu zinazohitajika mwilini na pia huongeza nguvu za kiume.

Mlonge una jumla ya virutubisho 92, mmea au mti mwingine wenye virutubisho vingi baada ya mlonge una virutubisho 28.

Pia, mlonge una viondoa sumu 46 na viondoa uvimbe mbalimbali mwilini 36, una asidi amino 18 na asidi amino muhimu zaidi tisa ambazo miili yetu haina uwezo wa kuzitengeneza.

Baadhi ya magonjwa ambayo unga wa majani ya mlonge, mbegu au mizizi una uwezo wa kutibu ni kisukari, shinikizo la juu la damu, matatizo au maumivu ya mishipa, pumu na hutuliza wasiwasi.

Magonjwa mengine ni maumivu ya kichwa, maumivu wakati wa hedhi, unasafisha mkojo na kibofu cha mkojo, unarekebisha matatizo kwenye tezi na huondoa mtoto wa jicho.

Namna ya kutumia unga wa mlonge

Kunywa kijiko kimoja (kijiko cha chakula) kutwa mara mbili, unaweza kuchanganya kwenye uji, chai au katika maji ya uvuguvugu.

Kiwango cha dozi kinaweza kuongezeka au kupungua kutegemea na hali ya mgonjwa.

Uwezo wa mti wa mlonge kutibu magonjwa mengi unatokana na kuwa na vitamini, madini mbalimbali na viondoaji sumu vingi kuliko mmea mwingine wowote.

Watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi (VVU) katika sehemu nyingi za Afrika Magharibi, ambao wanatumia mlonge ili kujikinga na magonjwa nyemelezi wameripotiwa kuongezeka kutokana na kuonyesha mafanikio kwa waliotumia awali.

Matatizo mengi ya kiafya yanatokana na viini lishe duni au hafifu, hivyo unapotumia tiba mbadala unakuwa unatibu magonjwa mbalimbali.

Mwandishi wa makala haya ni mtaalamu wa tiba mbadala