Faida za majani ya mkunazi

Friday February 8 2019

 

Mkunazi ni mti wenye faida mno ,mara nyingi huota maeneo ya ukanda wa Pwani.

Majani yake ndiyo dawa ya magonjwa mengi pamoja na yale yatokanayo na uchawi.

Magonjwa ya kichawi

Hapa labda itakushangaza kusikia dawa ya kutibu magonjwa ya kichawi.

Uchawi ni nguvu za giza ambazo hazionekani kwa macho.

Hali ambayo imeleta mkanganyiko kwa watu kugawanyika makundi mawili, moja linaamini uchawi upo na wengine wanaamini haupo na pia kuamini ni itikadi potofu.

Endapo una mgonjwa amepimwa lakini ugonjwa haukuonekana na amepewa dawa na ugonjwa unazidi badala ya kupona au kupata nafuu, hapo inaonyesha mgonjwa ana ugonjwa unaotokana na uchawi.

Au, akinywa dawa anazoshauriwa hazimponyi.

Mgonjwa yeyote mwenye hali hizi mbili atumie majani ya mkunazi.

Majani ya mkunazi yanatibu magonjwa mengi yatokanayo na uchawi, ni bora kuuotesha mti huu nyumbani kwako kama ulivyo otesha miti mingine.

Maandalizi yake

Chukua majani ya mkunazi yaanike kivulini, kisha yasage yawe unga laini. Tia kijiko kimoja kwenye maji kikombe kimoja mara tatu kwa siku 15.

Au, yaoshe majani mabichi na uyasage hadi yalainike iwe kama juisi. Kunywa kikombe kimoja mara tatu kwa siku 15.

Mimina kikombe kimoja cha juisi ya mkunazi kwenye maji kisha uoge kwa siku 15.

Majani ya mkunazi yanatibu vidonda vya tumbo

Vidonda hutokana na sababu nyingi sana kama kukaa muda mrefu bila kula chakula.

Tiba

Saga majani ya mkunazi kisha chota kijiko kimoja, chukua unga wa Habbat Sauda kijiko kimoja, mdalasini wa kihindi kijiko kimoja na asali lita moja kisha changanya na ukoroge vizuri. Kisha kunywa vijiko viwili kutwa mara tatu

Yatumieni majani ya mkunazi ikiwa ni mabichi au makavu kwa tatizo lolote la muda mrefu ambalo madaktari wameshakukatia tamaa ya kupona.

Mwandishi wa makala haya ni daktari wa tiba mbadala.