Hii ndiyo dawa ya kuua minyoo

Minyoo ni tatizo linalosumbua watu wengi sana na inaambukiza kirahisi.

Katika safu hii ya tiba mbadala tutajifunza namna ya kutibu tatizo la minyoo.

Kama ilivyo tiba mbadala ni rahisi na nzuri na gharama yake ni nafuu.

Minyoo ni wadudu warefu ambao wanaweza kuishi ndani ya tumbo la binadamu endapo wakifanikiwa kuingia.

Madhara ya minyoo

Kuna madhara mengi yatokanayo na minyoo ikiwamo kukonda mwili, kuwashwa, kukosa hamu ya kula au kula sana.

Pia, inaweza kukusababishia saratani ya utumbo.

Mwaka 2015, Shirika la Habari ya Uingereza (BBC), liliripoti kuwa kijana mmoja huko Marekani alipata saratani kwa kuambikizwa na minyoo.

Pia, kuna mwanamume alifariki dunia kwa kuambukizwa saratani na minyoo.

Tukio hilo liligunduliwa baada ya ushirikiano kati ya wanasayansi nchini Uingereza na Marekani.

Mwanamume huyo mwenye umri wa miaka 41 alidhaniwa kuwa anaugua vidonda vya kawaida vya tumboni lakini baada ya uchunguzi wa kina akagundulika kuwa na vidonda kwenye mapafu, maini na viungo vingine muhimu mwilini mwake.

Kituo cha uzuiaji na udhibiti wa magonjwa ya kuambukiza (CDC) cha Marekani, kimeripoti kuwa uvimbe wa mabuu kwenye ubongo yaani ‘neurocysticercosis’ hutokea baada ya mtu kumeza mayai madogo yanayosambazwa kupitia kinyesi cha mtu mwenye minyoo.

Mayai hayo yakiwa mwilini huangua minyoo inayoweza kuingia kwenye ubongo.

Tiba

Minyoo inaweza kutibiwa kwa kitunguu saumu. Unachotakiwa kufanya ni kumenya kitunguu saumu na kujaza kwenye kikombe kidogo cha kahawa.

Vitwange au saga kwenye blenda kisha mimina maji nusu lita.

Mchanganyiko huo unakunywa nusu kikombe cha chai kutwa mara tatu kwa siku tano hadi saba.

Mwandishi wa makala haya ni daktari wa tiba mbadala