Juisi ya miwa nzuri kwa wenye kisukari

Juisi ya miwa imetengeneza ajira hasa kwa vijana katika maeneo mbalimbali hapa jijini Dar es Salaam.

Licha ya kuwa biashara inayowasaidia wauzaji kiuchumi, pia ina faida nyingi kiafya.

Juisi inayotokana na miwa ina sukari halisi na watu wenye kisukari wamekuwa na uoga sana kutumia juisi ya miwa, kimsingi juisi hii ina faida nyingi sana katika mwili kwa wenye kisukari na kwa wasio na kisukari.

Juisi ya miwa ni chanzo cha vitamin, virutubisho na madini mbalimbali muhimu katika mwili,kama vile madini ya chuma na potassium, calcium, magnesium na manganese ambayo yana utajiri wa alkali inayosaidia kutoa hatari ya kupata maradhi ya saratani ya matiti kwa wanawake, saratani ya tezi dume na ya kibofu cha mkojo.

Juisi wa miwa husaidia sana utendaji kazi wa figo, moyo, ubongo na kwa wanaume husaidia sana kurekebisha mfumo wa utengezaji wa nguvu za kiume kwa sababu kuthibiti ongezeko la kiwango cha protini katika mwili.

Juisi ya miwa huimarisha kinga ya mwili, husaidia kulinda ini kupatwa na maambukizi mbalimbali na pia watoto na watu wazima hushauriwa sana kutumia juisi ya miwa kuwalinda na maradhi ya homa ya manjano.

Kiwango kikubwa cha madini ya potassium katika juisi ya miwa husaidia usagaji wa chakula, kwa hiyo kwa wenye tatizo la kukosa choo na wanaopata choo kigumu, juisi ya miwa au ulaji wa miwa ni dawa tosha na pia huzuia maambukizi katika tumbo pamoja na utumbo.

Mbali na kuwa nzuri kwa wagonjwa hao, inaelezwa kuwa

juisi ya miwa ikichanganywa na maji ya nazi au dafu huweza kutumika kupunguza maumivu katika via vya uzazi yanayotokana na maambukizi ya magonjwa ya ngono (STDs) na pia kusaidia kupunguza hatari ya tatizo la mawe katika figo (Kidney Stone). Kiasi kikubwa cha aina ya madini yanayopatikana katika juisi ya miwa husaidia sana kuzuia meno kuoza na kung’oka, huzuia fizi kutoa damu na hukata harufu mbaya ya kinywa.

Mwandishi wa makala hii ni muelimishaji namMshauri lishe kwa wagonjwa wa kisukari