Miamba 32 yapangiwa makundi

Monday September 1 2014

Monaco, Ufaransa. Ratiba ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ilipangwa wiki iliyopita mjini Monaco, Ufaransa na ikionyesha mechi za hatua hiyo ya makundi zitaanza kuchezwa Septemba 16 na 17, mwaka huu.

Ratiba hiyo inaonyesha mechi za hatua ya 16 bora zitachezwa mwezi wa pili mwakani na hatua ya mtoano itachezwa kuanzia mwezi wa nne na mechi ya fainali itachezwa Juni 6, 2015 mwakani kwenye Uwanja wa Olimpiki mjini Berlin, Ujerumani.

Makundi yaliyopangwa mwishoni mwa wiki iliyopita ni kama ifuatavyo:

Kundi A: Atletico Madrid, Juventus, Olympiakos, Malmo

Kundi B: Real Madrid, Basel, Liverpool, Ludogorets Razgrad.

Kundi C: Benfica, Zenit St Petersburg, Bayer Leverkusen, Monaco.

Kundi D: Arsenal, Borussia Dortmund, Galatasaray, Anderlecht

Kundi E: Bayern Munich, Manchester City, CSKA Moscow, Roma.

Kundi F: Barcelona, Paris St-Germain, Ajax, APOEL Nicosia.

Kundi G: Chelsea, Schalke, Sporting Lisbon, Maribor

Kundi H: Porto, Shakhtar Donetsk, Athletic Bilbao, BATE Borisov.

Advertisement