Mchezaji wa rugby akutwa amefariki

Monday August 19 2019

 

Mchezaji wa mchezo wa rugby akutwa akiwa amefariki, baada ya kucheza kwa mara ya kwanza akiwa na timu yake ya Batley Bulldogs.

Klabu hiyo imesema kwamba inasikitishwa sana na kifo cha Archie Bruce, mwenye umri wa miaka 20.

Mwenyekiti wa klabu hiyo alisema kuwa, timu ya Batley Bulldogs, itasaidia familia hiyo.

Bruce, ambaye hapo awali alikuwa akiichezea klabu ya Amewur ya Dewsbury Moor huko West Yorkshire, alicheza kwa mara ya kwanza katika timu hiyo baada ya kukaa nje kwa muda, huku akiipatia ushindi wa mabao 46-0 siku ya jumamosi.

"Habari za kusikitisha sana tunatoa rambirambi zetu za dhati kwa familia, marafiki pamoja na pamoja na wachezaji wa timu zote (Batley na Dewsbury Moor) pumzika kwa amani Archie.'' ilisema England,pia, St Helens imempendekeza Alex Walmsley, kushika nafasi ya Archie.

Klabu hiyo ilitoa rambirambi zao za dhati kwa familia yake, marafiki na kilabu, na kuongeza: "Tutajitahidi kwa kiasi chetu kuwaunga mkono.

Advertisement

By Amina Salum

Sources; DAILY NATION

Advertisement