Kiyombo amnyima usingizi kocha Singida United

Thursday June 7 2018

 

By GIFT MACHA

Kocha mpya wa Singida United, Hemed Morocco ameweka wazi mshambuliaji wake mpya, Habibu Kiyombo angekuwa amesajiliwa kwa mashindano ya SportPesa Super Cup, wasingefika hatua ya penalti na AFC Leopards.

Kiyombo aliyefunga mabao 17 katika mashindano yote msimu uliopita, amejiunga na Singida United kutoka Mbao, lakini ameshindwa kuitumikia timu hiyo kwa kuwa hakusajiliwa kwenye michuano hiyo.

Singida United imetinga nusu fainali kwa mikwaju ya penalti 4-2 dhidi ya AFC Leopards, jambo ambalo Morocco anaamini kuwa kama Kiyombo angekuwepo wangemaliza mchezo ndani ya dakika 90.

“Nilimpanga Kiyombo kwenye kikosi changu lakini baadaye nikaambiwa hawezi kucheza kwa kuwa hajasajiliwa kwenye mashindano haya. Kwetu imekuwa ni pigo maana ndiye straika tuliyekuwa tunamtegemea.

“Pamoja na yote tunashukuru kwamba tumetinga nusu fainali. Tunakwenda kucheza na timu ngumu ya Gor Mahia, tutajipanga vizuri,” alisema kocha huyo wa zamani wa Zanzibar Heroes.

Advertisement