Kocha Djuma apagawa ushindi wa Simba

Friday January 19 2018

 

Kocha Msaidizi wa Simba, Masoud Djuma ameingia kwenye rekodi ya kuwa mwalimu mwenye hisia kali kutokana na kuonyesha mihemko ya hali ya juu wakati timu yake inapokuwa uwanjani.

Kocha huyo Mrundi ambaye jana alikuwa uwanjani kukiongoza kikosi cha Simba, alikuwa ni mtu asiyetulia sehemu moja huku akionyesha hisia zake kwa ishara mbalimbali huku akigeuaka kuwa kivutio kwa mashabiki uwanjani hapo.

Mrudi Djuma anafahamika zaidi kwa mihemko yake hasa timu yake inapokuwa inacheza. Huonyesha hisia mbalimbali kwa ishara za mikono jambo ambalo huenda siku moja akakosea na kurusha ngumi bila kutarajia.

Djuma alionekana akiwa ameinama nje ya Uwanja akisali kila timu yake ilipopata mabao

Advertisement