Mastaa watano Ulaya walivyopiga pesa za usajili Ligi Kuu England

Ligi Kuu England maarufu kama EPL, imerejea tena baada ya miezi mitatu kupita huku vigogo wa ligi hiyo, wakiwa na silaha mpya ambazo wamesajili majira haya ya kiangazi.

Majira haya ya kiangazi imetumika jumla ya Pauni 1.41bilioni kwa usajili uliofanywa na timu zote za Ligi Kuu England wakinyemelea rekodi ya mwaka 2017 kwa mujibu wa Deloitte ambapo ilitumika Pauni 1.43 bilioni.

Wale vigogo wa ligi hiyo peke yao kwenye kiasi hicho cha fedha, wametumia Pauni 170 milioni katika siku 17 za mwisho ya usajili hicho ni kiasi kidogo cha fedha ukilinganisha na awamu zilizopita za majira ya kiangazi.

Arsenal awamu hii, wameonakana kutotaka mchezo majira haya kwa kwa kutumia Pauni 155milioni.Siku ya mwisho ya usajili, walimchukua beki wa kushoto wa Celtic, Kieran Tierney kwa Pauni 25 milioni na walitoa Pauni 8milioni kwa Chelsea ili wamnase beki wa kati, David Luiz.

Wakati ukishusha pumzi na kujaribu kupata picha msimu huu utakuwa na ushindani kiasi gani kutokana na usajili uliofanywa majira haya ya kiangazi hawa ni mastaa watano ambao wamesajiliwa kwa vitita vikubwa vya fedha.

Harry Maguire

Maguire mwenye umri wa miaka 26, ameweka rekodi ya kuwa beki ghari zaidi duniani baada ya kujiunga na Manchester United kwa Pauni 80 milioni akitokea Leicester City.

Rio Ferdinand ambaye aliwahi kutamba akiwa na Manchester United, anaamini beki huyo, anaweza kuongeza ubora kwenye safu ya ulinzi ya timu hiyo ambayo ilikuwa ikisuasua.

Nicolas Pepe

Uhamisho wa Pepe kutua Arsenal kwa ada ya Paundi 72 milioni umeweka rekodi ya kuwa mchezaji ghari zaidi kunaswa na washika mitutu hao wa London pia anashika nafasi ya pili kipindi hiki cha usajili nyuma ya Maguire.

Pepe ambaye amefunga mabao 35 katika michezo 74 ya Ligue 1 tangu amejiunga na timu hiyo, akitokea Lille, anasema imemchukua muda mrefu kupata nafasi ya kujiunga na klabu kubwa kama Arsenal.

“Kuwa hapa inanigusa sana,” anasema Pepe. “Nimepita njia ndefu na nilipitia changamoto nyingi, lakini malipo yake ni haya ya kupata nafasi ya kucheza kwa klabu hii.”

Rodri

Rodrigo Hernandez Cascante ni ingizo jipya kwenye kikosi cha Pep Guardiola ambaye usajili wake umeigharimu Manchester City Pauni 63 milioni, anakuwa miongoni mwa wachezaji ghali msimu huu.

Akimzungumzia kiungo huy, Kelvin De Bruyne, anasema mchezaji huyo ni mzuri kutokana na kucheza naye kwenye michezo kadhaa ya kujiandaa na msimu huu, ukiwemo ule wa Ngao ya Jamii dhidi ya Liverpool.

“Anaonekana tayari kuzoea staili yetu ya uchezaji, ni kitu ambacho hata kocha anahitaji naamini ni mchezaji sahihi kwetu, anayeweza kuongeza nguvu katika mpango wetu wa kutetea ubingwa wa ligi,” anasema De Bruyne.

Joao Cancelo

Cancelo ni beki wa kushoto aliyeigharimu Manchester City Pauni 60milioni kutoka Juventus, anatazamiwa kuja kutumika kama beki wa kulia katika nafasi hiyo, atakutana na Kyle Walker.

“Natambua kama Kyle ni mmoja ya mabeki bora wa kulia, nimekuja hapa kwa sababu napenda changamoto,” anasema Cancelo.

Tanguy Ndombele

Mara baada ya kutua kwenye kikosi cha Tottenham, Tanguy Ndombele kwa rekodi ya Pauni 54 milion akitokea Lyon, Dele Alli amefunguka kuwa anasubiri kwa hamu kucheza na kiungo huyo.

Mastaa waliotua kwa vigogo wa Ligi Kuu England ukiachana na hao ghari tukianza na Arsena, William Saliba (Saint Etienne, 27m), Kieran Tierney (Celtic, 25m), David Luiz (Chelsea, 7m), Gabriel Martinelli (Ituano, 6m), Dani Ceballos (Real Madrid, 15m - mkopo).

Chelsea Mateo Kovacic (Real Madrid, 40m). Manchester City ,Angelino (PSV, 5.3m), Morgan Rogers (West Bromwich Albion, 4m) na Scott Carson (Derby County, mkopo). Manchester United, Aaron Wan-Bissaka (Crystal Palace, 50m) na Daniel James (Swansea City, 17m).

Tottenham, Ryan Sessegnon (Fulham, 25m), Jack Clarke (Leeds United, 11.5m), Kion Etete (Notts County, imefichwa ) na Giovani lo Celso (Real Betis,mkopo).

Liverpool, Sepp van den Berg (PEC Zwolle, 4.4m), Adrian (West Ham United, bure) na Harvey Elliott (Fulham).