Mo Dewji aongeza nguvu Taifa Stars

Muktasari:

  • Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) limeunda kamati maalumu ambayo itahusika katika kuhakikisha kwamba timu ya Taifa Tanzania inafanya vizuri katika mchezo wao ujao dhidi ya Uganda.

IKIWA watanzania wakiwa wanataka kuona timu yao ikisonga mbele katika mashindano ya kufuzu Mashidano ya Mataifa Afrika yatakayofanyika Cameroon, tayari Shirikisho la mpira wa Miguu nchini (TFF) limeteua kamati ya kuhamasisha timu ya Taifa Tanzania kufanya vizuri.

Stars wanakabiliwa na mchezo muhimu dhidi ya Uganda utakaopigwa  mwezi ujao jijini Dar es salaam, mchezo ambao Stars inahitaji pointi ili iweze kusonga mbele katika mashindano hayo.

Hata hivyo katika kuhakikisha kwamba wanapata ushindi katika mchezo, tayari imeundwa kamati maalum ambayo itahusika katika kuhakikisha Stars inashinda katika mchezo huo.

Kamati hiyo imewahusisha Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam, Paul Makonda, Mohammed Dewji, Farouk Barhoza, Mohammed Nassor, Patrick Kahemele, Abdallah Bin kleb, Tedd Mapunda, Philimon Ntaihaja, Farid Nahid, Faraj Asas, Jerry Muro, Haji Manara na Eng. Hersi Said (KATIBU).

Katika kamati hiyo hawajaangalia upande wa klabu yoyote kwani umeunganisha utanzania baada ya kuwaweka kwa pamoja baadhi ya wadau wa klabu mbalimbali.