Ronaldo chupuchupu kwenda jela miaka miwili

Muktasari:

Mshambuliaji huyo Mreno alikuwa akikabiliwa na kosa la kuficha taarifa zake za mapato yatokanayo na mikataba yake ya matangazo na hivyo kukwepa kodi.

Mshambuliaji wa Juvetus, Cristiano Ronaldo ameepuka adhabu ya kifungo cha miaka miwili jela baada ya mahakama kumuamuru alipe faini ya dola 3.57 milioni za Kimarekani kwa kosa la kukwepa kodi wakati akiichezea klabu ya Real Madrid ya Hispania.
Mahakama hiyo ilimuhukumu Ronaldo kifungo cha miaka miwili ambacho muda mfupi baadaye kilipunguzwa na kuwa faini ya euro 365,000, ambayo inaongezewa katika faini nyingine ya euro 3.2 milioni, kwa mujibu w ahukumu hiyo.
Msemaji wa mahakama alisema haikuweza kufahamika mara moja kama faini hiyo itaongezewa katika euro 18.8 milioni ambazo Ronaldo alikubali kuilipa mamlaka ya kodi ya Hispania katika makubaliano yaliyofikiwa Juni mwaka jana.