Scholes ataja magonjwa matatu Man United

Kiungo wa zamani wa Manchester United, Paul Scholes ametaja maeneo matatu ya kuimarisha katika timu hiyo ambayo kwa sasa anaona inacheza kama “kikundi cha watu wasiofahamiana”. Bao pekee la penalti la Anthony Martial liliwapa ushindi Mashetani Wekundu wa 1-0 dhidi ya Partizan nchini Serbia katika Ligi ya Europa na kuhitimisha mwendo wa siku 232 bila kushinda ugenini.

“Hatuna Na. 10 wa ukweli, anayeweza kusambaza pasi na kufunga pia.

Tunahitaji pia kiungo anayezunguka uwanja wote, anayeunganisha mabeki na washambuliaji na pia Na.9 mwenye uchu.”