#WC2018: Russia yapiga mbili fasta

Thursday June 14 2018

 

Moscow, Russia. Wenyeji wa Kombe la Dunia, Russia wameanza vizuri mashindano hayo baada ya kwenda mapumziko wakiwa mbele kwa mabao 2-0 dhidi ya Saudi Arabiakwenye Uwanja wa Luzhniki, Moscow.

Wenyeji walianza mchezo huo kwa kasi na kufanikiwa kupata bao la kuongoza dakika 12 lililofungwa na Iury Gazinsky akitumia vizuri makosa ya mabeki wa Saudi Arabia.

Dakika 23, wenyeji Russia wamepata pigo baada ya nyota wao Alan Dzagoev kuumia na kushindwa kuendelea  mchezo huo nafasi yake kuchukuliwa na Denis Cheryshev.

Cheryshev aliwasahaulisha machungu Russia baada ya kufunga bao pili dakika 43, akiwalamba chenga mabeki wa Saudi Arabia na kupiga shuti lilojaa wavuni.

Matokeo hayo yanawaweka vizuri wenyeji kabla ya kuanza kipindi cha pili pamoja na mechi zao zinazokuja za Kundi A.

Advertisement