Zitto akutana na Samatta

Tuesday February 13 2018

 

By Haika Kimaro

Kiongozi wa chama ACT Wazelendo, Zitto Kabwe amemtembelea nahodha wa Taifa Stars na KRC Genk, Mbwana Samatta nyumbani kwake nchini Ubelgiji.

Zitto alikwenda nchini humo kwa shughuli za kichama na kupata fursa ya kuonana na mbuge mwenzake na mwenyekiti wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Tundu Lissu anayeendelea na matibabu.

Zitto alisema amefurahi kumsalimu na kumjulia hali Samatta kwani amemkuta akiwa mzima akishiriki mazoezi ya timu yake bila matatizo.

“Nimefurahi kupita kumsalimu na kumjulia hali Samatta, nimefurahi zaidi kumkuta akiwa mzima wa afya na anashiriki mazoezi ya timu yake bila shida,”alisema Zitto.

Aidha alisema inatia moyo zaidi kuona kijana wa Kitanzania anavyofanya kazi kwa bidii ili kufanikiwa zaidi na muombea Mola amuwezeshe kutimiza ndoto zake.

Samatta alijiunga na KRC Genk akitokea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) ambapo awali alikuwa akiichezea Simba SC.

Advertisement