Wadau wa Michezo waipongeza Tigo- Kili half marathon kwa kuibua vipaji.

Moshi. Waday wa riadha mkoani Kilimanjaro wamepongeza mchango mkubwa unaofanywa na Mbio maarufu Afrika mashariki za Tigo Kili Half Marathon katika kuibua vipaji mbalimbali vya wanariadha wanaoiwakilisha vyema nchi ya Tanzania katika Medani mbalimbali za Mashindano ya Mbio kitaifa na kimataifa.
Wakizungumzia namna mbio hizo zimesaidia kuinua vipaji vya wanariadha waliofanya vyema katika Mashindano ya Mbio kitaifa na Kimataifa kama vile Emmanuel Giniki na Alphonce Simbu; wadau hao wanafafanua kuwa, Tigo Kili Half Marathon imewaibua wanariadaha wengi mmashuhuri na ina mchango mkubwa katika kukuza mchezo wa ridaha nchini.
Mbio za Tigo-Kili Half Marathon zilizozinduliwa hivi karibuni mjini Moshi na wadau mbalimbali kutoka katika mataifa mbalimbali duniani wanatarajiwa kumiminika mkoani Kilimanjaro. Mbio hizo zinatarajiwa kuleta neema kubwa ya kiuchumi mkoa huo.
Mbio hizo zilizozinduliwa rasmi katika viwanja vya Kibo Palace Homes, mjini Moshi kwa kuwashirikisha viongozi mbalimbali, wadhamini, Chama Cha riadaha mkoani Kilimanjaro (KAAA), waandaaaji wa mbio hizo na wadau mbalimbali zinatarajiwa kufanyika siku ya jumapili ya Machi 1, 2020 katika viwanja vya Chuo Kikuu Cha ushirika mjini Moshi (MoCU).
Akizungumzia namna mbio hizo zimesaidia kuinua vipaji vipya ikiwemo Wanariadha wapya waliofanya vizuri katika mashindano ya kitaifa na kimataifa, Mwenyekiti wa Chama Riadha Maniaspaa ya Moshi (MMAAA), Abdi Massawe anasema kuwa kwa kutambua mchango mkubwa unaofanywa na Tigo Kili Half Marathon, chama chake kimepeleka wakimbiaji mahiri 17 kushiriki mashindano hayo ya kilometa 21 kwa mwaka huu wa 2020.
 
“Pia tutapeleka wakimbiaji mbalimbali zaidi ya 60 kutoka katika makundi mbalimbali ikiwemo wakimbiaji binafsi na Jogging klabu mbalimbali zilizoko mkoani Kilimanjaro kushiriki mashindano ya Tigo Kili Half Marathon…” alisema Abdi Massawe.
Massawe amewataka wananchi mbalimbali mkoani hapa kujitokeza kwa wingi kushiriki mashindano ya Tigo Kili Half Marathon kwani mbali na kuibua vipaji mbalimbali vya wanariadaha wapya, pia yatawasaidia kuboresha afya zao kupitia michezo.
 
Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa  Tigo Kanda ya Kaskazini, Aidan Komba alisema: “Tigo tunajivunia kuwa wadhamini wakuu wa mbio maarufu za Tigo Kili Half Marathon kwa mwaka wa nne mfululizo. Tukiongoza sokoni kwenye mageuzi ya maisha ya kidijiti yakiwamo masuala ya fedha, tunafurahi kwa mara nyingine tena kuwezesha usajili na malipo kwa washiriki kwenye mashindano hayo yajayo kupitia kwa huduma zetu kamilifu za fedha - Tigo Pesa.  
 
Alisema kwamba kwa miaka kadhaa sasa, Tigo Pesa imethibitishwa kuwa bora zaidi na mfumo wa kuaminika wa malipo kwa wanariadha wote wenye nia kutoka sehemu yoyote nchini.  “Zaidi ya hapo, tunakaribisha kila mmoja kwa ajili ya kupata kumbukumbu za mashindano hayo na kutumia wengine kupitia mtandao wenye kasi zaidi Tanzania wa 4G+,” akasema.
 
“Washiriki waendelee kujisajili kupitia mtandao na kufanya malipo kwa kutumia credit card kupitia  www.kilimanjaromarathon.com  au kupitia TIGO Pesa,” alisema na kuongeza kwamba washiriki wajisajili mapema ili kuepuka usumbufu. Usajili utafungwa Februari 16,2020 au nafasi zitakapojaa.