AS Vita yaiadhibu Simba mabao 5-0

Saturday January 19 2019

 

Timu ya Simba imepoteza mchezo wake wa pili hatua ya makundi baada ya kukubali kipigo cha mabao 5-0 dhidi ya AS Vital.

Mabao ya mapema ya AS Vital yaliwekwa dakika ya Makusi 14'  Bpunga 18 na Fabrice Ngoma 45 kipindi cha kwanza.

Mabao mawili ya AS Vital yaliwekwa wavuni kipindi cha pili huku wakionekana kulifikia lango la Simba mara kwa mara.

Mchezo huo ulionekana mkali huku Paschal Wawa na Jonas Mkude wakipewa kadi za njano.

Kocha wa Simba Patrick Aussems alimtoa Cleoutus Chama na nafasi yake kuchukuliwa na Dilunga dakika ya 61.

Katika D AS Vital ipo nafasi ya pili ikiwa na alama 3 huku ikifuatiwa na Simba yenye alama 3 ikizidiwa mabao ya kufunga na kufungwa.

Advertisement