Agrey Morris, Meddie Kagere chupuchupu wazichape uwanjani

Tuesday May 14 2019

By Michael Matemanga

Shughuli ya beki wa Azam, Agrey Morris kuwadhibiti mastraika wa Simba imesababisha, Meddie Kagere kupandwa na hasira katika mechi yao ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam jana Jumatatu.

Agrey Morris mara nyingi amekuwa akiwatoa nje ya mchezo washambuliaji wengi pindi anapokabiliana nao, hali inayosababisha washambuliaji hao kugombana naye au kulalamika kwa waamuzi.

Hali iyo ilijitokeza tena katika mechi yao dhidi ya Simba, baada ya kuonekana akitunishiana msuli na mshambuliaji, Meddie Kagere wa Simba baada ya kumchezea rafu mshambuliaji uyo.

Wachezaji hao walionekana wakitupiana maneno na kutaka kushikana, lakini busara za wachezaji wenzao Haruna Niyonzima wa Simba na Nico Wadada wa Azam ndio ziliepusha balaa ilo ambalo hata mwamuzi pamoja na wachezaji wengine hakuwa akiwaona.

Beki wa Azam Nico Wadada baada ya kuona tukio ilo aliamua kwenda kumshika mkono Agrey Moris na kumsihi asimfate mshambuliaji huyo baada ya kutupiana maneno, huku naye Haruna Niyonzima wa Simba aliamua kumsihi Meddie Kagere aondoke asigombane.

 

Advertisement