Al Hilal yapata kocha mpya

Muktasari:

  • Baada ya kupokea kichapo cha 2-1 kutoka kwa Nkana, Uongozi wa Al Hilal umeamua kumtimua kocha wao ili waweze kupata mtu sahihi atakae waweka kwenye ramani.

Dar es Salaam. Klabu ya Al Hilal ya Sudan imepata kocha mpya Nabil Kouki raia wa Tunisia ili kuziba pengo la Irad Zaafouri aliyetimuliwa baada ya kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa Nkana Fc.

Al Hilal inayoshiriki kombe la Shirikisho Afrika, ilichezea kichapo hicho nchini Zambia dhidi ya Nkana inayochezea Mtanzania, Hassan Kessy.

Magoli ya Walter Bwalya wa Nkana, yaliweza kuharibu kabisa kibarua cha Irad na kumfanya akifungishiwa virago baada ya kuonekana hana mipango thabiti katika timu hiyo.

Hii ni mara ya 3 kwa kocha Kouki kuifundisha Al Hilal, baada ya kufanya hivyo mwaka 2015 na 2017 na hivi saa amerejea tena katika kikosi hicho kwaajili ya kuokoa jahazi.