Amunike ataka ushindi mapema kwa Uganda

Tuesday March 19 2019

 

KOCHA wa timu ya Taifa Stars, Emmanuel Amunike  ameonyesha kuhitaji zaidi soka la haraka katika kikosi chake.

Katika mazoezi yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Boko Veterans, Amunike alianza kwa kutengeneza programu ya kucheza mpira kwa kasi.

Aligawa timu mbili huku akisisitiza kila mchezaji kutokaa na mpira mguuni badala yake akipata mpira awe mwepesi wa kuachia kwa mchezaji mwenzake na kusonga mbele.

Vilevile alikuwa anawataka wachezaji wake wajue kujipanga pindi wanapokuwa na mpira huku wale wasiokuwa na mpira pia wawe makini katika kukaba.

Zoezi hilo lilionekana kueleweka na wachezaji hao, hivyo haikuwa ikimchukua muda kocha huyo kubadili programu kila dakika zilivyokuwa zinaenda.

Wachezaji waliokuwa mazoezini, Kipa Aish Manula (Simba), Metacha Mnata (Mbao Fc), Suleman Salula (Malindi Fc), Hassan Kessy (Nkana, Zambia), Vicent Philipo (Mbao Fc) , Gadiel Michael (Yanga), Ally Mtoni (Lipuli), Aggrey Morris (Azam), Kelvin Yondani (Yanga), Erasto Nyoni (Simba).

Wengine ni Kennedy Wilson (Singida), Himid Mao (Petrojet) Mudathir Yahya (Azam), Feisal Salum (Yanga), Yahya Zayd (Ismaily), John Bocco (Simba), Shiza Ramadhan (Ennpi), Rashid Mandawa(Bdf) na Simon Msuva (Al Jadida).

Advertisement