Aussems asaini mwaka mmoja Simba

Sunday May 26 2019

 

By THOBIAS SEBASTIAN

UONGOZI wa Simba chini ya Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Mohammed Dewji 'Mo Dewji' ulimsanisha mkataba mpya wa mwaka mmoja kocha wao Mbelgiji Patrick Aussems kutokana ule wa awali kuelekea ukingoni mwisho wa msimu huu.
Kilicho pelekea Aussems kusainishwa mkataba mpya ni kufanya vizuri katika yale matakwa yaliyokuwa katika mkataba wa awali ambayo yalikuwa kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu Bara jambo ambalo alilifanikisha na lingine ilikuwa ni kufika katika hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika ambalo nalo walivuka na kufika hatua ya robo fainali.
Mwenyekiti wa Simba Swedy Mkwabi alisema wamemsainisha Aussems mkataba mpya kutokana alifanya vizuri kwenye yale malengo yaliyokuwa katika mkataba wa awali na wanaimani nae kubwa msimu huu ataifanya timu yao iweze kung'ara zaidi ya msimu huu.
"Mkataba aliosaini ni wa mwaka mmoja ambao ninamatumaini makubwa ataifanya timu kuwa imara na kufika mbali zaidi ya msimu uliopita katika mashindano yote kwani mkataba huu mpya una malengo zaidi ya ule ambao umemalizika," alisema Mkwabi.
Aussems alisema mkataba mpya utakuwa na malengo zaidi ya ule msimu uliomalizika yaani katika mashindano yote jambo ambalo atahakikisha analifanyia kazi na kulifanisha hilo msimu ujao.
"Tutafanya maandalizi mazuri kuanzia katika (Pre Season) kwa kupata mahala sahihi ambapo kila mchezaji ataandaliwa katika njia sahihi lakini tutafanya usajili wa kuongeza nguvu katika timu kulingana na mapungufu ambayo yalijitokeza msimu uliopita," alisema Aussems.

Advertisement