Azam kuivaa Gor Mahia bila Chilunda

Wednesday July 11 2018

 

By THOMAS NG’ITU

STRAIKA Shaban Chilunda anakosekana katika kikosi kinachocheza na Gor Mahia  mchana huu baada ya klabu ya Tenerife kukamilisha baadhi ya vitu ambavyo vilikuwa vimesalia katika mkataba wake.

Azam itashuka dimbani kukipiga na Gor Mahia katika mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Kagame Cup leo saa nane mchana katika Uwanja wa Taifa.

Chilunda alisaini mkataba wa miaka miwili wa kuitumikia timu hiyo inayoshiriki Ligi Daraja la Pili nchini Hispania, huku akiwa ni mchezaji wa pili baada ya Farid Mussa kwenda awali katika timu ya vijana katika klabu hiyo hiyohiyo.

Awali Chilunda alikaririwa na Mwanaspoti kwamba anaweza kuondoka nchini muda wowote kwani kuna vitu vidogo ambavyo ndivyo vilimfanya achelewe kuondoka nchini kwani Tenerife walikuwa bado hawajamkamilishia.

Kikosi cha Azam kitakachocheza na Gor Mahia  Razack Abarola, Nicco Wadada, Bruce Kangwa, Abdallah Kheri, Aggrey Morris,Mudathir Yahya,Joseph Mahundi,Frank Domayo,Ditram Nchimbi,Salum Aboubacary na Ramadhan Singano.

Advertisement