Azam yatangaza kikosi cha kuivaa Triangle United, Ngoma, Chilunda waanzia nje

Sunday September 15 2019

 

Dar es Salaam. Washambuliaji Donald Ngoma na Shaban Idd Chilunda wameanzia benchi wakati Azam FC ikishuka uwanjani kusaka ushindi dhidi ya Triangle United katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika leo saa 10:00 jioni kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi.

Katika mchezo huo kocha Ettiene Ndayiragije ameamua kuwaweka benchi Ngoma na Chilunda akiwaanzisha nyota wake Richard Djodi na Obrey Chirwa.

Tangu Ndayiragije atue Azam msimu huu Ngoma ameshindwa kupata namba katika kikosi cha kwanza cha mabingwa hao wa Kombe la FA.

Chirwa na Djodi wameonyesha maelewana mazuri tangu mchezo uliopita dhidi ya Fasil Kenema ambao Azam ilishinda nyumbani.

Katika eneo la kiungo Frank Domayo leo ataanza pamoja na Salum Abubakar wakiwa na jukumu la kuilinda ngome yao huku wakipitisha pasi za mwisho kwa washambuliaji wao.

Kikosi cha Azam: Razack Abarola, Nico Wadada, Bruce Kangwa, Daniel Amoah, Yakub Mohamed, Frank Domayo, Salum Abubakari, Idd Seleman ‘Nado’, Richard Djodi, Obrey Chirwa na Emmanuel Mvuyekure.

Advertisement

Wachezaji wa akiba Mwadini Ally, Mudathir Yahya, Idd Kipagwile, Donald Ngoma, Masoud Abdallah, Shaban Chilunda na Oscar Masai.

Advertisement