Babu wa miaka 74 asajili kucheza ligi ya Misri

Muktasari:

Klabu ya daraja la tatu ya 6th October FC imemsajili Eez Eldin Bahder akiwa babu wa umri miaka 74.

Cairo, Misri.Shirikisho la Soka la Misri (EFA) limetangaza kupokea usajili wa mchezaji mzee zaidi katika historia ya soka la kulipwa duniani.

Klabu ya daraja la tatu ya 6th October FC imemsajili Eez Eldin Bahder akiwa babu wa umri miaka 74, akitarajia kuanza kuichezea timu hiyo hivi karibuni.

Hakuna taarifa ya ziada iliyotolewa kuhusu mkataba wa Bahder na klabu hiyo.

Babu huyo hajulikani katika rekodi za wachezaji wa soka Misri kwa sababu hakuna klabu yoyote kubwa aliyochezea kabla.

Hivyo EFA na Badher imewakaribisha Guinness Book of World Records kwenda kushuhudia mechi ya daraja la tatu ili kuona babu huyo akicheza soka lake la kulipwa akiwa na umri mkubwa zaidi.