Bayern yaifanyia kweli Liverpool

Muktasari:

  • Liverpool imeshindwa kutamba licha ya kucheza nyumbani kwenye Uwanja wa Anfield dhidi ya Bayern Munich.

London, England. Licha ya kucheza kwenye uwanja wake wa nyumbani Liverpool, imeshindwa kupata pointi tatu dhidi ya Bayern Munich.

Liverpool ikiwa Anfield ilibanwan na Bayern katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp alisema ndoto yake ilikuwa kupata pointi tatu katika mchezo huo ingawa amevutiwa na kiwango cha wachezaji wake.

Klopp alisema hawezi kutoa lawama kwa wachezaji  kutokana na matokeo hayo ingawa alidai ndoto yake haikutimia.

“Tumefanya siku yetu kuwa ngumu ingawa tulicheza vizuri,” alisema kocha huyo wa zamani wa Borussia Dortmund.

Alisema kipindi cha kwanza walicheza kwa kiwango bora na walipoteza idadi kubwa ya nafasi za kufunga mabao.

Bayern yenye maskani Allianz Arena, Ujerumani imecheza michezo tisa bila kufungwa katika mashindano hayo.

Licha ya kumiliki mpira, Bayern Munich haikupiga shuti langoni mwa Liverpool kwa mara ya kwanza katika Ligi ya Mabingwa  Ulaya tangu mwaka 2015 ilipocheza na Barcelona.