Bingwa mbio za mita 100 duniani kupinga kufungiwa

Muktasari:

Coleman amefungiwa kushiriki riadha miaka miwili kutokana na kugundulika kutumia dawa za kusisimua misuli ambazo zimekatawa michezoni.

Paris, Ufaransa (AFP). Bingwa wa dunia wa mbio fupi, Christian Coleman atakata rufaa kupinga adhabu ya kufungiwa miaka miwili kutokana na kukiuka sheria zinazokataza matumizi ya dawa za kusisimua misuli, meneja wake amesema leo Jumatano Oktoba 28.

"Uamuzi wa Mahakama ya Nidhamu iliyoundwa chini ya sheria za Chama cha Riadha Duniani, haukubaliki na utakatiwa rufaa Mahakama ya Kimataifa ya Michezo," Emanuel Hudson aliandika katika akaunti ya Twitter ya kampuni yake ya HSI.

"Coleman cha zaidi cha kusema hadi wakati ambao shauri hilo linaweza kusikilizwa katika mamlaka za mahakama."

Coleman, ambaye alitwaa ubingwa wa dunia wa mbio za mita 100 mwaka jana jijini Doha akitumia muda unaoongoza duniani wa sekunde 9.76s, awali alifungiwa kutokana na kutoonekana mara tatu mwezi Juni.

Mahakama ya Nidhamu ya Chama cha Soka Duniani ilikubaliana na mashtaka na kumfungia Mmarekani huyo mwenye umri wa miaka 24, kwa miaka miwili hadi Mei 14, 2020.

Kama adhabu hiyo ikiendelea, Coleman atakosa Michezo ya Olimpiki ijayo itakayofanyika Japan, ambako angekuwa mmoja wa watakaokuwa wanapewa nafasi ya kushinda medali ya dhahabu ya mbio za mita 100.