Bingwa wa Tenisi Sharapova ang’oka mashindano ya French Open

Thursday May 16 2019

 

Bingwa mara mbili wa mashindano ya French Open, Maria Sharapova amelazimika kujiondoa katika mashidano hayo kutokana na majeraha aliyopata.

Sharapova amelazimika kuondolea kwenye mashindano hayo kutoka na matatizo ya bega yanayomkabili.

Mrusi huyo amewahi pia kutwaa taji tuzo ya Gland Slam kwenye  halfa iliyofanyika Paris Ufaransa mwaka 2012 na 2014.

Nyota huyo aliandika kwenye ukurasa wake wa Instagram akielezea kujitoa  kwenye mashindano hayo makubwa duniani.

Aliandika kwenye Instagram akisema, “Kujitoa kwenye Mashindano ya French Open wakati mwingine  kufanya uamuzi kama huo sio jambo rahisi.”

Aliongeza kuwa hata hivyo habari njema amerejea kufanya maozezi mepesi ambayo taratibu yanamuwezesha kuanza kupata ahueni ya maumivu ya kwenye bega linalomsumbua.

Alimaliza kwa kuandika kuwa atawakumbuka washiriki wote  wa mashindano hayo yanayoendelea Paris, pia ni matarajio yake wataonana mwakani tena.

 

Advertisement