Cheki mtasha anavyojivunia kuichezea Serengeti Boys

Wachezaji wa Serengeti Boys wakifanya mazoezi kwenye viwanja vya JK Park,Dar es Salaam jana,wakijianda na mashindano ya Afrika ya vjana ya U-17 yanayoanza Aprili14 hadi28 jijini Dar es Salaam.Picha na Michael Matenga

Muktasari:

  • Starkie ambaye ni beki wa pembeni na aliamua kukubali kuichezea Serengeti Boys kwa kumfuata mama yake ambaye ni Mtanzania wa Mkoa wa Kilimanjaro na baba yake ni Mwingereza.

Dar es Salaam. Mzungu wa timu ya Taifa ya vijana chini ya miaka 17, ‘Serengeti Boys’, Ben Starkie aliyezaliwa nchini England ameweka wazi sababu zilizomshawishi kuichezea timu hiyo na amesisitiza watafanya maajabu katika mashindano ya Afcon.

Starkie ambaye ni beki wa pembeni na aliamua kukubali kuichezea Serengeti Boys kwa kumfuata mama yake ambaye ni Mtanzania wa Mkoa wa Kilimanjaro na baba yake ni Mwingereza.

Alisema, sababu kubwa ya kurudi kuichezea Serengeti Boys kwa sababu ya kipeumbele ambacho Tanzania wamempa na anajivunia kwa nafasi hiyo.

“Kikubwa ni kipaumbele kwa Taifa la Tanzania na najisikia furaha kuwa miongoni mwa kikosi kinachounda Serengeti Boys. Kitu ambacho nitafurahi zaidi kukiona ni namna Serengeti Boys itakavyofanya vizuri kwenye michuano hii,” alisema Starkie.

Starkie ambaye anachezea akademi ya Lugbytown ya England alisema, pamoja na kuichezea Serengeti Boys hana mpango wa kujiunga na klabu yoyote ya Tanzania kwani mpango wake ni kuchezea moja ya timu kubwa England.