Chelsea yafutiwa kusajili madirisha mawili

Muktasari:

  • Pia, Chama cha Soka England (FA) nacho kumejikuta kikilimwa adhabu kwa kutozwa Pauni 391,260.

Klabu ya Chelsea imefungiwa kusajili kwa madirisha mawili msimu ujao kutokana na kukiuka kanuni za usajili wa  wachezaji chini ya miaka 18.

Hivyo Shirikisho la Soka Duniani limetoa adhabu hiyo kutokana na kushindwa kufuata kanuni za usajili kifungu namba 19 cha Fifa. Pia Chelsea imepigwa faini ya Pauni 460,314.

Pia, Chama cha Soka England (FA) nacho kumejikuta kikilimwa adhabu kwa kutozwa Pauni 391,260.

Taarifa iliyotolewa na Fifa ilieleza kwamba Kamati ya Nidhamu ya Fifa imeiadhibu klabu ya Chelsea na Chama cha Soka England kwa kuvunja kanuni za kimataifa za uhamisho na usajili wa wachezaji chini ya miaka 18.

Hivyo kamati hiyo imeiadhibu Chelsea kutosajii wachezaji wapya kikosini hapo iwe kwa mchezaji wa ndani au wa kimataifa.

Chama cha Soka England licha ya kutozwa faini kipewa muda wa miezi sita kujieleza kuhusu usajili wa kimataifa   kusajili wachezaji wa nyongeza.