Chelsea yakaribia Man United

Tuesday February 13 2018

 

Klabu ya Chelsea imeiduwaza West Brom baada ya kuitandika mabao 3-0 kwenye mchezo wa Ligi Kuu England ulipigwa jana Jumatatu usiku.

Ushindi huo umewasogezea Chelsea hadi nafasi ya nne wakiwa na pointi 53 wakiwa nyuma ya Man United kwa pointi tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu England.

Mabao mawili ya Eden Hazard na moja la Victor Moses yalitosha kuwapa ushindi huo mnono siku ya jana na kufufua matumaini kuwapo mbio za nafasi nne za juu.

 Chelse imepoteza mechi zake mbili zilizopita za EPL ambapo ushindi huo wa jana umewapa ari ya kuifukuzia Man United iliyopo nafasi ya pili.

Vipigo kutoka kwa Bournemouth na Watford vilimuweka pabaya kocha Antonio Conte ambaye hadi sasa bado hajaweka wazi hatima ya kibarua chake ambacho kimeonekana kuwa njiapanda.

Advertisement