Dani Alves atwaa taji la 40 ndani miaka 18 ya soka

Muktasari:

Alves alitwaa taji kwanza mwaka 2006 akiwa na Sevilla, aliyoichezea kwa miaka sita kabla ya kujiunga na FC Barcelona.

Dar es Salaam. Beki wa PSG na Brazil, Dani Alves baada ya kutwaa ubingwa wa Copa Amerika ameweka rekodi ya kuchukua taji lake 40 ndani ya miaka 18 ya kucheza soka la ushinda.

Alves alianza kuchea soka Brazil katika klabu ya Bahia kabla ya kujiunga na Sevilla 2002.

Beki huyo wa kulia mwenye umri wa miaka 36, ametwaa na taji matatu ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, akiwa na FC Barcelona kwenye miaka ya 2009, 2011 na 2015.

Pia katika mafanikio yake, alianza kutwaa ubingwa wa Copa Amerika, 2007 na Kombe la Mabara mara mbili katika miaka ya 2009 na 2013 kabla ya kuchukua tena Copa Amerika, Jumapili iliyopita.

Mafanikio aliyonayo katika uchezaji wake soka yanamfanya kuisogelea rekodi ya Muafrika, Hossam Hassan ndiye mchezaji mwenye mafanikio zaidi kwa kutwaa mataji mara 41.

Katika orodha ya wachezaji wenye mafanikio ya kutwaa mataji mengi zaidi ni Ibrahim Hassan (37), Maxwell (37 ), Oleksandr Shovkovskiy (36 ), Andres Iniesta (35 ),  Lionel Messi (35),  Ryan Giggs (35), Zlatan Ibrahimovic (35 ), Sir Kenny Dalglish (34) na Vitor Baia (34).