De Bruyne kuikosa Man United Jumatano
Muktasari:
- Kiungo huyo Mbelgiji alipata jeraha Jumamosi iliyopita wakati wa mechi ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya dhidi ya Tottenham Jumamosi iliyopita.
Kiungo wa Manchester City, Kevin De Bruyne hatacheza mechi ya kesho ya vigogo wa jiji hilo itakayofanyika Old Trafford, kwa mujibu wa kocha wake Pep Guardiola.
Kiungo huyo Mbelgiji alipata jeraha lake jingine msimu huu wakati alipolazimika kutoka uwanjani katika mechi ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya dhidi ya Tottenham iliyoisha kwa vigogo hao wa Ligi Kuu kuibuka na ushindi.
"Ni tatizo la misuli," Guardiola amewaambia waandishi wa habari leo Jumanne. "Bado tutaangalia katika siku zinazofuata lakini kwa kesho hatacheza."
Man City inaweza kukamata usukani wa Ligi Kuu na kuongoza kwa tofauti ya pointi moja iwapo itaibuka na ushindi kesho na itafanikiwa kutetea ubingwa iwapo itashinda mechi zake tatu za mwisho.
Msimamo wa Ligi Kuu ya England ni kama ifuatavyo:
# Team MP W D L F A D 1. Liverpool 35 27 7 1 79 20 +59 88 2. Manchester City 34 28 2 4 87 22 +65 86 3.Tottenham 34 22 1 11 64 35 +29 67
4. Chelsea 35 20 7 8 59 38 +21 67 5. Arsenal 34 20 6 8 68 43 +25 66 6. Man United 34 19 7 8 63 48 +15 64
7. Everton 35 14 7 14 50 44 +6 49 8. Watford 34 14 7 13 49 49 +0 49 9. Leicester City 35 14 6 15 48 47 +1 48 10. Wolves 34 13 9 12 41 42 -1 48 11. West Ham 35 12 7 16 44 54 -10 43
12. Crystal Palace 35 12 6 17 43 48 -5 42 13. Newcastle 35 11 8 16 35 44 -9 41
14.Bournemouth 35 12 5 18 49 62 -13 41 15. Burnley 35 11 7 17 44 62 -18 40
16. Southampton 34 9 9 16 40 57 -17 36 17.Brighton & Hov 34 9 7 18 32 53 -21 34
18. Cardiff City 35 9 4 22 30 65 -35 31 19. Fulham 35 6 5 24 33 76 -43 23 20. Huddersfield 35 3 5 27 20 69 -